Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

KOCHA, Ole Gunnar Solskjaer amesema kwa sasa hana uhakika tena wa kuhusu kiungo Paul Pogba kama ataendelea kubaki kwenye kikosi cha Manchester United.

Ripoti zilizotoka Hispania zimedai kwamba Real Madrid wameonyesha dhamira ya dhati ya kumnasa kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa ambaye kwa sasa amekuwa na kiwango cha hovyo huko Old Trafford

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa kabla ya mechi dhidi ya Chelsea itakayofanyika kesho Jumapili huko Old Trafford, Solskjaer alisema: "Huwezi kuwa na uhakika wa kila kitu kwenye soka.

"Lakini, ndio nadhani Paul ataendelea kuwapo hapa. Nataka kuwaambia, mipango yake ipo kwenye kufanikiwa United."

Hata hivyo, ripoti zimedai kwamba Pogba mwenyewe amedaiwa kuwaambia wachezaji wenzake kwamba haoni kama Man United itapata maendeleo yoyote hasa chini ya kocha huyo na hilo ndilo linalochochea uwezekano wa staa huyo kuhama timu hiyo.
 
Watu wengi ambao wako katika mahusiano mbalimbali wanayo tabia ya kununiana pale wanapokwaza. Wako wengine wanaonuniana kwa sababu tu ya kuambiwa ukweli na mwenzake. Labda amemuonya katika jambo fulani, akawa amechukia kuambiwa ukweli huo hivyo anaanza kumnunia tena bila hata kuongea naye.
 
Imekuwa ni kawaida kwa watu wengi kwenye mahusiano kununiana pale wanapokuwa wamekosana. Kwangu mimi kununiana na mtu ni ujinga, chuki na wivu na sababu binafsi ndiyo zinapelekea haya yote kutokea lakini kama ingekuwa tunachukulia tu poa mambo kama haya yasingeweza kutuyumbisha.
 
Bosi wako, hutakiwi kumnunia bosi wako. Bosi hakosei, anafanya kile anachokitaka hivyo kumnunia bosi wako ni ujinga wa hali ya juu. Mtu anayekusaidia maisha yako yaende siyo mtu wa kumnunia au kumchukulia poa. Mtu ambaye anamnunia bosi wake huenda akili yake haiku sawa hivyo anatakiwa akapimwe.
 
Bosi wako ndiyo mteja wako namba moja kama umeajiriwa. Hivyo basi, unatakiwa kumfanyia mambo mazuri bosi wako mpaka afurahi na siyo kumnunia. Kumnunia mtu anayekusaidia kukupatia kipato cha kuweza kuendesha maisha yako ni mtu unayepaswa kumweshimu sana.
 
Unatakiwa ujitume sana katika yoyote ile unayopewa na bosi wako, hata kama imekwisha omba tena majukumu mengine. Kazi yako wewe ni kufanya kazi bora za kumshangaza bosi wako kwa utendaji mzuri wa kazi. Na ukishampendeza bosi wako ataweza kukulipa vizuri kwa sababu unampa thamani nzuri kwenye kazi yake.
 
Mtu wa pili ni mteja wako. Kama uko kwenye biashara hutakiwi kumnunia mteja wako. Iko falsafa ya mteja ambayo inasema kuwa mteja hakosei na mteja yuko sahihi muda wote. Unatakiwa kumwacha mteja afanye kile anachotaka kwa sababu katika biashara yako yeye ndiyo bosi.
 
Inapotokea mteja wako amekwenda kununua sehemu nyingine hupaswi kumnunia tena anapokuja kurudi kwenye eneo lako la biashara mfurahie kwa kurudi kwake. Mpatie tena huduma bora sana ambayo hatoweza kuipata sehemu nyingine yoyote ila kwako tu.
 
Hatua ya kuchukua leo; usiwanunie watu hawa wawili, moja bosi wako na pili mteja wako. Uwaheshimu kwa sababu hao ndiyo wanafanya maisha yako yaende mbele na biashara yako iende. Bila hao watu hakuna maisha katika mahusiano yetu.
 
Kwahiyo, jenga mahusiano bora kati ya wewe na mteja wako na bosi wako pia. Wape thamani bora sana na siku zote usiwanunie bali wachekee, kumnunia mteja na bosi wako ni sawa na kukataa fedha. Unapokataa fedha maisha yako yatakuwaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…