KOCHA, Ole Gunnar Solskjaer amesema kwa sasa hana uhakika tena wa kuhusu kiungo Paul Pogba kama ataendelea kubaki kwenye kikosi cha Manchester United.
Ripoti zilizotoka Hispania zimedai kwamba Real Madrid wameonyesha dhamira ya dhati ya kumnasa kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa ambaye kwa sasa amekuwa na kiwango cha hovyo huko Old Trafford
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa kabla ya mechi dhidi ya Chelsea itakayofanyika kesho Jumapili huko Old Trafford, Solskjaer alisema: "Huwezi kuwa na uhakika wa kila kitu kwenye soka.
"Lakini, ndio nadhani Paul ataendelea kuwapo hapa. Nataka kuwaambia, mipango yake ipo kwenye kufanikiwa United."
Hata hivyo, ripoti zimedai kwamba Pogba mwenyewe amedaiwa kuwaambia wachezaji wenzake kwamba haoni kama Man United itapata maendeleo yoyote hasa chini ya kocha huyo na hilo ndilo linalochochea uwezekano wa staa huyo kuhama timu hiyo.