Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis hii leo amekutana na wasusi, wanamitindo na wataalam wa mitindo ya ulimbwende mjini Vatican, lakini akawaonya dhidi ya kuwa na udaku ama umbea wakati wakiwa wanaendesha shughuli zao za kikazi.
Papa Francis amewataka wahudumu hao wa saluni kufanya kazi zao kwa njia ya Kikristo na kuwatendea wateja wao kwa heshima na upole.
 
Kila wakati ongeeni na wateja wenu kwa unyenyekevu na muwape matumaini katika maisha," amesema Papa na kuongeza; "mjitahidi kujizuia na vishawishi vya kuanziasha maongezi ya udaku ambayo ni rahisi kufanyika katika mazingira ya kazi yenu."
Papa amewataka wahudumu hao kuiga tabia njema za mtakatifu na mlezi wa waumini wa kanisa hilo wanaojihusisha na masuala ya urembo, Martino de Porres, aliyeishi Peru katika karne ya 16.
 
De Pores aliishi jijini Lima na alikuwa kinyozi shughuli ambayo kwa kipindi hicho ilihusisha pia kufanya upasuaji wa kukata viungo.
Mtakatifu huyo anatajwa kufanya miuziza kadhaa ikiwemo kutibu kwa haraka, kuongea na wanyama, kuwa sehemu mbili kwa wakati mmoja na kunyanyua watu juu bila ya kuwashika.
 
Lakini je hilo lina ukweli? mwandishi wa BBC Lizzy Masinga amemuuliza swali hilo Asnath Mwalukunga, anayemiliki Asnath Salon jijini Dar es Salaam na kusema: "kuna ukweli kiasi chake katika hilo lakini si kweli kuwa wahudumu wote ni wambea. Mimi huwakataza wafanyakazi wangu kuanzisha mada za udaku na kusengenya watu. Lakini nashindwa kufanya hivyo kwa wateja wangu. Naheshimu wateja, sitaki kuwapoteza."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…