Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hatua ya kwanza ya kuwa na maisha yenye furaha ni kujua nini hasa unachotaka, wapi unakotaka kufika, kisha kujua njia sahihi ya kufika unakopata kufika. Ukishajua unachotaka na ukaijua njia sahihi, kazi yako ni kukaa kwenye njia hiyo sahihi na kuweka juhudi mpaka ufike unakotaka kufika.
 
Chagua mtu ambaye ameshafika kule unakotaka kufika wewe, na mtumie kama kiongozi wako, kama mtu utakayejifunza kwake kupitia hatua alizopiga mpaka kufika kule alikofika, ambapo ndiko unataka kufika wewe pia.
 
Ukishajua njia sahihi, unapaswa kukaa kwenye njia hiyo na kuepuka njia nyingi zinazotamanisha utakazokutana nazo mbele yako. Maana wengi watakuja kwako na njia zinazoonekana ni nzuri, lakini zitakuwa siyo njia sahihi kwako.
 
Ili kuwa na maisha yenye furaha, unapaswa kufanya kile ambacho ni sahihi na muhimu kwako kufanya, na siyo kufanya kile ambacho kila mtu anafanya. Unapaswa kuwa tayari kwenda kinyume na kundi kubwa la watu, kwa sababu mara nyingi kinachofanywa na wengi siyo kilicho sahihi. Kuwa tayari kusimama mwenyewe na kwenda kinyume na kile kinachofanywa na kila mtu.
 
Tafuta kitu ambacho ni kuzuri kwa ndani na siyo chenye mwonekano mzuri wa nje. Watu wengi huwa wanahangaika na mwonekano wa nje, lakini ndani kunakuwa tupu. Wewe kazana na uzuri wa ndani na siyo mwonekano wa nje pekee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…