Jambo hilo linafanya kuwapo na matukio ya kuvunjwa kwa rekodi za usajili karibu kila mwaka na kuonekana kama vile ni ngumu sana kumpata mchezaji mzuri kwa bei ya kutupa.
Wakati klabu nyingi zikilazimika kutumia pesa nyingi kusajili wachezaji zinaowataka, unaambiwa hivi sasa kuna wachezaji hao wapo vizuri kwelikweli na wanapatikana kwa bei ya kutupa kutokana na vipengele vilivyowekwa kwenye mikataba yao.
Beki wa kati, Kostas Manolas atakumbukwa daima na mashabiki wa AS Roma kama ataamua kuachana na timu hiyo mwishoni wa msimu huu. Beki huyo Mgiriki ni moja ya wakali wanaosakwa kwelikweli huko Ulaya.
Lakini, utashangaa kwenye mkataba wake kuna kipengele kinachosema kwamba kama kutakuwa na timu itakayokuwa tayari kulipa Euro 36 milioni basi ruhusa kuvunja mkataba huo. Wakati mabeki wengine kama Virgil van Dijk na Aymeric Laporte wakipatikana kwa pesa nyingi, Manolas ni rahisi sana na ubora wake ni uleule kama wa wakali hao.
Kiungo huyo mshambuliaji alienda kujiunga na Villarreal kwenye majira ya kiangazi mwaka 2017 baada ya Malaga kushuka daraja. Tangu wakati huo, Pablo Fornals amefunga mabao tisa na kuasisti mara 19 kwenye La Liga na Europa League katika mechi alizoitumikia Villarreal.
Kiungo huyo amekuwa kwenye rada za timu nyingi ikiwamo Napoli na Arsenal, lakini kubwa ni baada ya kufahamika kwamba mkataba wake una kipengele kinachotaja pesa ndogo sana kama unahitaji huduma yake. Euro 30 milioni tu zinatosha kumnasa Fornals, mchezaji mwenye ubora mkubwa ambaye kimsingi angepaswa kuuzwa kwa dau kubwa zaidi.
Mbelgiji, Toby Alderweireld amejitengenezea jina kubwa kwenye Ligi Kuu England na kuwa mmoja wa mabeki bora kabisa akitamba huko kwenye kikosi cha Tottenham Hotspur. Kwa kuwa na huduma yake, Spurs imekuwa moja ya timu zenye ukuta mgumu kwenye ligi, huku akicheza kwa kutengeneza pacha matata kabisa na Mbelgiji mwenzake, Jan Vertonghen.
Lakini, ubora wote huo wa ndani ya uwanja, Toby anapatikana kwa pesa ndogo sana kwa timu inayotaka kumsajili baada ya mkataba wake kuwa na kipengele kinachohitaji kulipiwa Euro 29 milioni tu kwa timu inayotaka kumsajili.
Huduma yote hiyo matata, lakini mkataba wa Iglesias una kipengele kinachobainisha saini ya mchezaji huyo inaweza kupatikana kwa kulipia Euro 28 milioni tu na ndio maana klabu nyingi vigogo vinafukuzia saini yake.
Ever Banega ni bonge la kiungo na kuna wakati alihusishwa sana na Arsenal kwamba walikuwa wakifukuzia huduma yake. Kiungo huyo wa Kiargentina anacheza soka lake huko Sevilla na hakika siku zote amekuwa akicheza soka la kiwango cha juu.
Banega amefunga mabao manne na kuasisti mara mbili kwenye Europa League wakati kwenye La Liga amefunga mabao matatu na kuasisti mara nne. Amekuwa akifanya vyema pia shughuli yake ya kukaba na kupiga pasi matata.
Lakini, huwezi kuamini kwamba huduma bora yote hiyo ya Banega unaweza kuipata kwa Euro 20 milioni tu kama ilivyobainishwa kwenye moja ya vipengele vilivyopo katika mkataba wake huko Sevilla.