Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kufanya makubwa kwa baadhi ya timu na kuboronga kwa hata zile zilizotarajiwa kufanya vyema kumesababisha msimamo ulivyo, ambapo kama si miujiza basi ni dhahiri kwamba Manchester City, Liverpool, Chelsea na Tottenham Hotspur watafuzu kwa UCL.
 
Wanaume wamejituma, lakini wengine wamepoteza nafasi na mechi muhimu sana, hasa Arsenal na Manchester United ambao sasa lao ni kurudi kwenye Ligi ya Europa, lakini Arsenal bado wana matumaini ya kushiriki iwapo watatwaa ubingwa wa Ligi ya Europa.
 
Ubingwa England bado ni kizungumkuti kwa sababu Liverpool wana alama 94 kutokana na michezo 37 wanachauana vikali na Manchester City ambao (kabla ya mechi yao ya jana usiku dhidi ya Leicesrer City) walikuwa na alama 92 kwa michezo 36 hivyo bado ngoma hapo ni mbichi na hakuna anayejua nani atachukua kombe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…