Mapendekezo hayo ni pamoja na uboreshaji wa huduma ya kwanza viwanjani. Marefa walitakiwa kuwalinda wachezaji mara wanapoona amejeruhiwa vichwani ndiyo maana husimamisha mpira na kuita watoa huduma ya kwanza haraka.
Mara nyingine hata X-Ray huweza kutumika kubaini kama mfupa wa fuvu la kichwa umepasuka. Kama kuna damu imevuja huweza kuonekana kirahisi na hatua za kuiondoa damu hiyo kwa njia za upasuaji hufanyika haraka.
Mpaka kufikia leo taarifa za madaktari wa Liverpool zinaonyesha mchezaji huyo yuko fiti kucheza mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu dhidi ya Wolves hapo keshokutwa.
Hata kama hatapangwa keshokutwa lakini ana uhakika wa kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Totenham itakayopigwa jijini Madrid Hispania Juni Mosi 2019.
Kadiri anavyopumzika ndivyo afya yake inavyoboreka, hivyo ni vizuri kujifunza kuwa mwenye majeraha kama ya Salah hupumzishwa baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina.