Pep Guadiola amewahakikishia Manchester City kuwa hana mpango wa wa kuacha kazi katika klabu hiyo kwa miaka miwili licha ya tetesi kuwa huenda akajiunga na Juventus msimu huu wa joto.(Express)
Manchester United wanamtaka kiungo wa kati wa Everton Idrissa Gueye,29. Everton inata karibu paunimilioni 40 kumuuza kiungo huyo wa kimataifa wa Senegal. (Mail)
Mesut Ozil, 30, hataondoka Arsenal msimu huu wa joto. Kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani atasalia Gunners hadi mkataba wake utakapokamilika.(Mirror)
Klabu ya Nice inayoshiriki League 1 inapania kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Olivier Girroud,32, msimu ujao, kwa mujibu wamkurugenzi wa kiufundi wa Gilles Grimandi.(Canal Footbal Club via Bleacher Report)
Kiungo wa kati wa Leister City mbelgiji YouriTielemans,22, anatarajiwa kurejea Monaaco baada ya uhamisho wake wa Foxes utakapomalizika (VTM Nieuws-kwa kidachi)
Vilabu vya Paris st-Germain na Atletico Madrid vinataka kumnunua msambuliaji wa Everton na kiungo wa Kimataifa wa Brazil Richarlison,22, ambaye bei yake inakadiriwa kuwa pauni milioni 70. (Mirror)
Everton wameanzisha mazungumzo na Barcelona kusu uhamisho wa kudumu wa wa kungo wa kati wa Ureno Andre Gomes,25, anayechezea klabu hiyo kwa mkopo(LiverpoolEcho)
Kumekua na mvutano mkubwa kati ya mshambuliaji wa Real Madrid, Gareth Bale na meneja Zinadine Zidane, kumaanisha kuwa kiungo huyo wa kimataifa wa Wales hana maisha katika klabu hiyo.(AS-in Spanish)