Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Man City iliichapa Brighton 4-1 kwenye mechi ya mwisho ya msimu na Liverpool wao waliichapa 2-0 Wolves na hivyo kumaliza vita hiyo ya ubingwa, ambapo mshindi akipatikana kwa tofauti ya pointi moja, 98 kwa 97.
 
Bingwa, timu zilizoshika Top Four zimepatikana na hata zilizoshuka daraja pia zimeshafahamika. Kwenye ligi hiyo kuna mgawo wa pesa, ambapo timu ya juu kwenye msimamo, inakuwa inapokea nyongeza ya kama Pauni 2 milioni tofauti na ile ya chini yake, hivyo hadi inayoshika mkia kwenye ligi.
 
Huddersfield Town kwa kushika nafasi ya mwisho kwenye msimamo, yenyewe imelipwa Pauni 1.9 milioni, wakati Fulham ya juu yake imepata Pauni 3.8 milioni, huku Cardiff City walioshuka daraja pia, lakini wao wameshika nafasi ya 18, wamepata mgawo wa pesa Pauni 5.8 milioni.
 
Bournemouth wao wamepata mgawo wa Pauni 13.4 milioni, wakati Newcastle United waliopo juu wamevuna Pauni 15.4 milioni na Crystal Palace wamepata Pauni 17.3 milioni, huku Watford kwenye nafasi ya 11 wamevuna Pauni 19.2 milioni na West Ham United waliokamatia nafasi ya 10, wamekusanya mkwanja wa Pauni 21.1 milioni.
 
Kwenye nafasi ya juu, Leicester City, wamevuna Pauni 23.1 milioni, wakati Everton kwenye nafasi ya nane wameweka kibindoni Pauni 25 milioni na Wolves nafasi ya saba imewafanya wavune Pauni 26.9 milioni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…