Beckham alisema alitaka kucheza mechi hiyo dhidi ya Chelsea akiwa amenyoa na alimficha Kocha Ferguson kwa wiki nzima kabla ya kuja kushtukiwa muda mfupi kabla ya mechi huko Wembley na kutakiwa kwenda kunyoa haraka.
Beckham alisema: “Tangu nilikuwa na umri wa miaka saba au nane, siku zote nilikuwa nataka kunyoa staili ya nywele ambayo wengine hawakuwa wakinyoa. Nilikuwa nikitaka kuvaa nguo tofauti na wachezaji wenzangu. Nilinyoa kiduku na nilikuwa naogopa kumwonyesha kocha.
Nilikuwa naenda mazoezini na kofia. Nafanya mazoezi nikiwa na kofia, naenda hotelini na kofia, tunakula chakula cha usiku na kofia, kifungua kinywa asubuhi bado nina kofia, hata kwenye basi tulilopanda kwenda uwanjani, nilikuwa na kofia.
Nikaanza kujiandaa na mechi, hapo nikavua kofia. Kocha akaona na kusema: ‘Nenda kanyoe haraka.’ Nikajichekesha na kama kugomagoma hivi, lakini akasema: ‘Niko siriazi, nenda kanyoe.’
.KINDA wa Chelsea, Callum Hudson-Odoi ameripotiwa kutaka apewe jezi yenye namba 10 inayovaliwa na Eden Hazard kwenye timu hiyo ikiwa ni sehemu ya masharti yake ili asaini mkataba mpya wa kubaki Stamford Bridge.
Kinda huyo alikaribia kabisa kutimkia Bayern Munich kwenye dirisha la Januari, lakini Chelsea iliamua kumbakiza baada ya kutambua kwamba watakabiliwa na adhabu ya kufanya usajili.
Chelsea imefungiwa kusajili na sasa ipo kwenye wakati mgumu kumshawishi Hazard abaki kwenye timu yao baada ya kudaiwa kuwindwa kwa nguvu zote na Real Madrid