Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wanamtazama waone atakachokifanya kwenye dirisha lijalo la usajili wa majira ya kiangazi kuinusuru timu hiyo. Ed Woodward ndiye makamu mwenyekiti wa Man United - ndiye anayehusika na mambo ya usajili, hivyo shughuli pevu inamkabili.
 
Man United isipopata wachezaji inaotaka kusajili, lawama zote kwake, hana pa kujificha. Ndiyo maana ngumu kuwa Ed Woodward kwa kipindi hiki. Anasukumwa na benchi la ufundi. Anasukumwa na mashabiki na anasukumwa na wamiliki wa timu. Presha kila kona.
 
Woodward tayari ameshabadili makocha mara nne ndani ya muda mfupi na kuitia timu hasara. Hivyo anahitaji kuwa na utulivu kwenye dirisha hili la usajili kupata mastaa watakaobadili hali huko Old Trafford. Man United imepoteza makali yake tangu iwe chini yake. Tofauti na ilivyokuwa kwenye enzi za David Gill.
 
Lakini anafeli kwenye usajili. Makocha watatu David Moyes, Louis van Gaal na Jose Mourinho wote wamekuja na kuondoka kwa kulipwa pesa nyingi za fidia. Anaelekea kwenye kumlipa fidia pia Ole Gunnar Solskjaer kama hatafanya usajili makini kwenye dirisha lijalo. Paul Pogba amemnasa kwa Pauni 89 milioni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…