Mchungaji James Ngβangβa awamwagia matusi maaskofu , awataka wamuheshimu mke wake, lasivyo atawatimua wote nchini Kenya | _ kanisa la Neno Evangelist Ministry amegonga vichwa vya habari kwa mara nyengine tena baada ya kutishia kufunga matawi ya kanisa lake la Neno Evangelism akidai kwamba maaskofu hawamuheshimu mke wake. Katika kanda ya video iliosambaa katika vyombo vya habari , anaonekana akiwakaripia maaskofu kwamba atawafurumusha wote iwapo hawataheshimu onyo lake akidai kuwa matawi hayo yamekuwa vibanda. βWakati huu nitawaonyesha uwezo wanguβ¦ mwanamke yeyote ambaye hatamuheshimu mke wangu β¦.mulinipata hapa na wake zenu, mumejitajirisha kupitia juhudi zanguβ . βWajinga nyieβ¦wajeuriβ¦nilikuwa nikihubiri katika mkokoteni , naapa mbele ya Mungu nitawaonyesha Ngβangβa ni naniβ¦.β. Kwa mujibu wa BBC. Mchungaji huyo anaonekana akiwaambia kwamba ni kinyume kwa wao kujigamba kuhusu utajiri waliojipatia kutoka katika kanisa lake na bado hawamuheshimu. βNataka kuwaambia nyinyi maaskofu, iwapo hamutamuheshimu mke wanngu nitawafurumusha katika kanisa langu. sitaki kujua wewe ni naniβ, alisema mchungaji huyo. Ngβnga anasema kuwa amefikisha umri ambao anahitaji kuheshimika na maaskofu wote. Ninapo kohoa lazima mutii, alisema. Mchungaji huyo alisema kuwa anakabiliwa na changamoto kwa sababu shetani anataka kuliangusha kanisa lake. βShetani anakabiliana nami kwa sababu anataka kuniangusha, hakuna kitu munachoweza kuniambiaβ¦.Mimi ni Neno na ndio maana ninapigwaβ¦. Sitawaruhusu nyinyi na wake zenu kunipatia msongo wa mawazo zaidiβ,alisema. βIwapo munataka kujiita maaskofu, munahitaji kufikiria kule mulikotoka, ni vipi munajigamba mbele yangu na mulikuja kwangu na umaskiniβ¦nitawafukuza nyie nyoteβ¦ takatakaβ, aliendelea. Amesema kuwa atayafunga matawi yote na kusalia na makao makuu pekee. Ngβangβa aliwataja maaskofu wake kuwa watu wasio na maana, wajinga na wasiomuheshimu kama mtu aliyewasaidia. βNi lazima waniheshimu la sivyo nitaelekea kuvifunga mimi mwenyewe vibanda vyote nibakie na kanisa kubwa lililopo jijini Nairobi. Mimi ndio mwanzilishi wa Nenoβ, alisema huku akipongezwa na wafuasi wake