Sina cha kuongezea shemeji...
Ila nisisitize tu kwamba kipindi hiki ndiyo nafasi nzuri sana kwa baba kuonyesha upendo wa kweli kwa mama watoto. Na huo muda wa kuchiti katika kipindi hiki utaupata wapi? Na utaweza kweli kufurahia huko nje wakati binti wa watu huku yupo na kitoto chako kichanga kimalaika anakusubiri?
Kabinti kangu kalizaliwa tukiwa mbali nje huko peke yetu bila wajomba, mashemeji wala ndugu. Nilijifunga vibwebwe nikamwambia mama wewe kula bata ngoja mimi nitekiova - kuanzia kumkanda, kumuogesha, kumpikia, kusafisha nyumba na hasa hasa sapoti ya kisaikolojia. Kumkumbusha kwamba tulikuwa tumebarikiwa sana kwa kujaliwa kamalaika haka. Kushiriki katika mpango mtakatifu wa uumbaji. Maneno matamu ya kumtia nguvu. Vizawadi vya mara kwa mara. Chakula akipendacho na alikuwa anapenda sana kukandwa miguu na mgongo. Mpaka nilijisomea na kuangalia video mbalimbali kuhusu massage ya miguu na mgongo. Na zaidi ya yote kila wakati kusali - hata kama ni visala vifupi vifupi tu vya shukrani, ulinzi na amani ya moyo. Nadhani hiki ndicho kipindi ambacho mapenzi yetu yaliimarika sana na actually yeye ndiye alianza kunionea huruma kuwa nateseka sana...na alipoanza tu kujisikia vizuri message za mgongo zile zikaanza kuzaa mengine (japo kwa polepole na uangalifu sana).
Shangazi yake alipokuja kumuona baada ya miezi mitatu hivi alimkuta keshanenepa anang'ara hata huwezi kujua kama ni mzazi. I real felt proud of myself and grew up as a man. Pure, deep unconditional love....Stella, toto jeupe legevu wewe...I really loved you baby girl ...and you will always remember me [emoji7][emoji7][emoji7][emoji8][emoji8][emoji8]