Ni kipindi ambacho ndoa inakuwa ngumu sana. Kwa upande wangu naona mwanaume ndiye anasababisha mwanamke ahamishie mapenzi kwa mtoto.
Mwanamke kama alitarajia kupata mimba, moja kwa moja penzi analipeleka kwa mtoto huku furaha(mapenzi na furaha ni vitu viwili tofauti) yake ikibaki kwa mume,na kama mume alitarajia hiyo mimba,atafurahia ujio wa mtoto,basi,baba atamkosha mke wake, mke atamshukuru Mungu kwa kupata mme mpenda familia, mke ataligawa penzi katikati, akitamani alipo yeye,mume na watoto wawepo pia. Kinyume chake, Furaha na mapenzi ni kwa watoto, baba atabaki kama baba/mume.
Suluhisho ni moja tu, mwanaume ahakikishe anafanya mapenzi na mke wake hadi siku anakaribia kujifungua. Kama akijifungua salama aanze nae wiki ya pili tangu ajifungue(ndomu muhimu) japo atalalamika lakini ataelewa.
Kuoga mara kwa mara kunamfanya mama achangamke, pia mume anatakiwa kumsaidia mke kazi za nyumbani na kumbembeleza mtoto, hii huongeza thamani ya mume kupendwa na kuthaminiwa.
Kutoka out na kichanga huwa inamfanya mke awe na amani sana.
Take away ya vyakula anavyo vipenda huwa vinaongeza mihemko kwa mwanamke.
Mume ajitahidi kumsimulia mke umbea hata wa uongo ili mradi utazibamba hisia zake...
Hayo yote hayatasababisha ndoa iwe na AMANI pasipo kumshirikisha Mungu kwa kila jambo.
Omba sana kwa Mungu akupe mwenza wa kufanana naye [emoji120][emoji120]