Wachezaji wanapaswa kutambua majukumu yao. Lakini imekuwa tofauti kabisa kama mchezaji hatakubali kufuata utaratibu milango iko wazi,” alisema kigogo huyo.
Washambuliaji Edinson Cavani na Luis Suarez wameiongoza Uruguay kupata ushindi wa kishindo cha mabao 4-0 dhidi ya wachezaji 10 wa Ecuador katika mchezo wa Copa Amerika.
Uruguay pia ilipata bao lililofungwa na Nicolas Lodeiro na lile la kujifunga kwa beki wa Ecuador, Arturo Mina katika mchezo wa Kundi C uliofanyika kwenye Uwanja wa Mineirao.
Uruguay ilianza kucheza na faida ya mchezaji moja zaidi katika dakika 24, baada ya nyota wa Ecuador, Jose Quintero kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumpiga kiwiko Lodeiro.
Uruguay ilikuwa inatawala mchezo huo wakati Quintero anatolewa nje kwenye Uwanja wa Mineirao, katika mchezo huo ulioshuhudiwa na mashabiki wachache 13,000.
Lodeiro alifunga bao la kwanza katika dakika sita akimalizia pasi ya Suarez akiwa ndani ya eneo la 18, kabla ya Cavani kuongeza bao la pili kwa shuti akimalizia mpira uliotemwa na kipa wa Ecuador, Alexander Dominguez katika dakika 33.