DHANA YA KUCHEZEWA
Inawezekana kila mmoja akachambua kwa mtindo wake, lakini mwisho maana inabaki katika mlengo mmoja tu, kupotezewa muda, kutumika kimapenzi! Hiyo ndiyo maana ya moja kwa moja.
Kama ndivyo, mwanaume ana kitu gani cha tofauti katika mwili na moyo wake, ili aondolewe kwenye kipengele cha kuchezewa na kuachwa? Wapo wanaume ambao maisha yao yamebadilika baada ya kuachana na wapenzi wao waliowapenda.
Hata wanaume nao huteswa, huteseka na hushindwa kufanya mambo mengine, pindi wanapochukua uamuzi mgumu wa kuachana na wale ambao wanawapenda kwa dhati.
HISIA
Naomba niwatoe mchanga machoni kuwa, hisia za mapenzi ni zile zile. Haina maana kwamba, mwanamke ana uwezo wa kupenda sana kuliko mwanaume, la hasha! Kikubwa ni hisia kuwa za kweli.
Kama ndivyo, mwanaume ana kitu gani cha tofauti katika mwili na moyo wake, ili aondolewe kwenye kipengele cha kuchezewa na kuachwa? Wapo wanaume ambao maisha yao yamebadilika baada ya kuachana na wapenzi wao waliowapenda.
Kwamba mwanamke kama atakuwa hajampenda mwanaume kwa dhati, kadhalika na mwanaume naye akiwa hajampenda mwanamke kwa dhati, itabaki kuwa hivyo, lakini kama wote watakuwa na mapenzi ya kweli, hali hiyo itaendelea kuwa hivyo kwa wote.
KUWEKEZA MAPENZI
Kama ulikuwa hujui, anza sasa kuingiza jambo hili kichwani mwako, kama wafanyabiashara wanavyowekeza katika sehemu mbalimbali, ndivyo ilivyo pia katika mapenzi.