Maelezo aliyoyatoa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni wiki chache zilizopita katika Bunge la Jamhuri ya Muungano kuhusiana, pamoja na mambo mengine, masheikh wa Zanzibar waliopo mahabusu katika gereza la Ukonga Dar es Salaam yamenikumbusha kisa hicho nilichokieleza hapo juu.
Nimejiuliza peke yangu, nikaona haitoshi, niulize na wenzangu akiwemo na yeye mwenyewe, hivi amelewa pombe gani iliyompelekea aeleze mambo ambayo hata mtoto mdogo anaweza kubaini kwamba ni ya kuhandisiwa?