Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wanasoka mahiri kama beki wa kati Sergio Ramos na straika matata, Harry Kane walitumia kipindi hiki cha majira ya kiangazi barani humo kula viapo vya ndoa na warembo wao wakiingia kwenye jukwaa la mume na mke kufurahia maisha mapya.
 
Majira haya ya kiangazi huko Ulaya yamekuwa ya kufurahia harusi za mastaa mbalimbali, ambapo supastaa wa Arsenal, Mesut Ozil naye alikuwa mwanasoka aliyeachana na ukapera wakati alipojibebea mrembo wake wa Kituruki, mwanamitindo Amine Gulse.
 
Hata hivyo, Ozil hakuwa staa pekee wa Arsenal aliyeoa katika majira haya ya kiangazi, baada ya kiungo mshambuliaji Henrikh Mkhitaryan naye kuaga ukapera kwa kufunga ndoa na mrembo wake kipenzi, Betty Vardanyan huko Venice, Italia. Miki aliyejiunga na Arsenal Januari mwaka jana akitokea Manchester United alionekana kuwa mwenye furaha wakati alipokamilisha harusi na asali wa moyo wake, mrembo Betty.
 
Kane yeye alijibebea kipenzi chake cha tangu enzi za utoto, mrembo Kate Goodland huku kila mmoja akionekana kuwa mwenye furaha kubwa kufurahia jambo hilo ambapo sherehe zake zilifanyika kwa mbwembwe kubwa. Kane na Kate walioana baada ya kuchumbiana kwenye visiwa vya Bahamas, huku wawili hao wakiwa wameanza kufahamiana tangu walipokuwa wadogo shuleni.
 
*Wakenya walimpeleka kwenye kambi ya timu ya taifa kuhamasisha wachezaji Donald Maliga mtu ambae ni legend wa soka la Kenya mtu ambae alishawahi kucheza fainali ya UEFA, wachezaji wanatamani kuwa kama yeye, hata alichokiongea pale kambini kinahusu football*.

*Sisi watanzania tumepeleka mwanasiasa kwenda kuhamasisha wachezaji, matokeo yake anaongea na wachezaji kuhusu ilani ya CCM na jinsi CCM itakavyokuwa inashinda kila siku*.

*Watanzania Mungu atusamehe tu.*
 
Kane na Kate wamefanikiwa kupata watoto wawili wa kike, Ivy na Vivienne. Kwenye harusi ya Ramos, baadhi ya mastaa waliohudhuria ni David Beckham na mkewe Victoria, Ronaldo de Lima, Roberto Carlos, Alvaro Morata sambamba na Luka Modric huku pia akiwepo kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane.
 
Wawili hao waliachana miaka miwili iliyopita baada ya kuanzisha uhusiano mwaka 2014, lakini walirudiana kwa kasi na kuamua kuoana kabisa. Mrembo Laura ni mwigizaji akiwa na umri wa miaka 46, alikubali kuolewa na Schmeichel mwenye umri wa miaka 55. Harusi yao ilifanyika katika Kanisa la Egebaeksvang, Espergaerde huko Copenhagen, Denmark ikiwa ni miezi minne tu imepita baada ya kuchumbiana.
 
Wawili hao waliachana miaka miwili iliyopita baada ya kuanzisha uhusiano mwaka 2014, lakini walirudiana kwa kasi na kuamua kuoana kabisa. Mrembo Laura ni mwigizaji akiwa na umri wa miaka 46, alikubali kuolewa na Schmeichel mwenye umri wa miaka 55. Harusi yao ilifanyika katika Kanisa la Egebaeksvang, Espergaerde huko Copenhagen, Denmark ikiwa ni miezi minne tu imepita baada ya kuchumbiana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…