Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

3. Mke pampas (Pampas wife)
Hawa ni wavivu sana na wameharibiwa na familia zao hasa zile familia tajiri.


Wake wa sampuli hii, hawawezi fanya kazi yeyote. Wanatuma hovyo hata waume zao, utasikia baby nipe hicho, baby njoo unitolee hiki. Kama kuna house girl au boy ni zaid ya punda kwao.
 
4. Mke ofisi
(The office wife)
Hawa husahau kabisa majukumu yao kwa kisingizio cha kazi. Wanajifanya bize muda wote na majukumu ya kiofisi kuliko hata familia. Wanawake wa aina hii mara nyingi huishia kwa waume wao kuporwa na ma-house girls
 
6. Mke Mwalimu Mkuu
(Headmistress)

Hawa hugeuka viranja mpaka ndani ya nyumba, hata kwa mume wake anajifanya muelekezi tu na humuuliza maswali: "Kwa nini hii hivi", mara "Hicho hapo sipo mahali pake" mbona "Mbona unatia sukari nyingi namna hiyo kwenye chai?" Tena hata bila kujali kuna nani, hata kama kuna mgeni.
 
7. Mke ngumi mkononi.
(Fighting wife)

Hawa muda wote ni wavarangati na akiamua kulianzisha, huwa hawaangalii mazingira na ataongea kama cherehani, bila mipaka. Ikitokea unaishi uswazi, basi kila jirani lazima atajua nyumbani kwako kumeharibika. Yuko radhi hata kukunjana na mume wake.
 
8. Mke Ndoo ya taka
(Dustbin wife)

Hawa huwa wachafu kupita maelezo, kiasi kwamba hawajali hiki cha thamani au vipi, utamkuta mchafu muda wote. Mara chache sana huhudhuria kwenye sherehe au shughuli za kijamii. Waume za wanawake wa aina hii huwachoka mapema.
 
9.Mke mlinzi
(Protective wife)

Hawa huwabana waume zao mpaka inafikia kuwa kero. Hujifanya ama wana wivu au wana wasiwasi kwamba waume zao watanyakuliwa na wanawake wengine. Hufikia mpaka kuwaona wanawake wote ni maadui wake na hawataki kuona hata marafiki wake wakiwa karibu na mume wake. Anahisi anaibiwa na ukirudi nyumbani, badala ya kupokea mzigo mkononi anakupokea simu iliyoko mfukoni
 
10. Mke mzuri
(A good wife)

Wanawake hawa ndio wale walioandikwa kwenye MITHALI 31 na vitabu vingine vya ndani ya Biblia. Hawa ni wapole wanyenyekevu, wasikivu hata kama amekosewa, anatumia busara kulitatua tatizo,
Hata hivyo, wanawake wa aina hii si wengi sana katika dunia ya leo.

Ewe Mwenyezi Mungu, wabariki wanawake wote walioko namba 10 na kama hawajaolewa wajaalie wapate waume bora.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…