Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kutokana na hili, yapo madaraja mbalimbali yaliyojengwa sehemu mbalimbali duniani ili kuboresha usafiri wa barabara na reli. Karibu uongeze maarifa yako kwa kufahamu madaraja 15 makubwa au marefu zaidi duniani kwa sasa.
 
Daraja la Danyang–Kunshan

Daraja la Danyang–Kunshan ndilo daraja refu kuliko yote duniani, lina urefu wa kilometa 164.8. Daraja hili linapatikana huko China kati ya Beijing–Shanghai na lilikamilika kujengwa mwaka 2010. Daraja hili hutumiwa na treni ya umeme inayokwenda kasi.
 
Daraja la Changhua-Kaohsiung

Changhua-Kaohsiung ni daraja la pili kwa urefu duniani linalopatikana huko Taiwan. Daraja hili lina urefu wa kilometa 157.3, lilikamilika mwaka 2007 na linatumiwa na treni ya umeme ya kasi kubwa.
 
Daraja la Tianjin



Daraja la Tianjin linaunganisha Langfang na Qingxian katika njia ya treni ya mwendokasi ya Beijing–Shanghai huko China. Daraja hili ni moja kati ya madaraja marefu duniani kwani lina urefu wa kilometa 113.7.
 
Daraja la Cangde


Daraja hili limejengwa kwenye njia ya treni ya kasi kubwa ya Beijing – Shanghai huko China. Daraja hili lina urefu wa kilometa 105.8 na limejengwa kwa mfumo ambao linaweza kustahimili matetemeko; lilikamilika mnamo mwaka 2010.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…