Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mfaransa, Kylian Mbappe ni mkali mwingine ambaye saini yake imemaliza pesa nyingi za watu, akihama kutoka AS Monaco tu na kutua PSG, lakini hapo imelipwa Euro 180 milioni, huku Mbrazili mwingine, Philippe Coutinho saini yake kuanzia Vasco da Gama, Inter Milan, Liverpool hadi sasa akikipiga Barcelona, imegharimu kiasi cha Euro 174 milioni.
 
Angel Di Maria saini yake si mchezo, imetafuna pesa nyingi na kuziingizia klabu mkwanja mrefu, alipohama kutoka Rosario Central, Benfica, Real Madrid, Manchester United na PSG, huduma yake ikigharimu Euro 169.2 milioni, huku Ousmane Dembele akiingia kwenye orodha hiyo kwa saini yake kugharimu Euro 160 milioni, akinaswa kutoka Rennes, Borussia Dortmund na sasa akikipiga huko Barcelona.
 
Straika Zlatan Ibrahimovic, amepita kwenye vikosi vya Malmo, Ajax, Juventus, Inter, Barcelona, AC Milan, PSG, Manchester United na sasa yupo huko Marekani, kote alikipita huko huduma yake imegharimu Euro 159.5 milioni, huku staa mpya wa Barcelona, Antoine Griezmann akiingia kwenye orodha baada ya saini yake kugharimu Euro 150 milioni. Akinaswa kutoka Real Sociedad, Atletico Madrid na sasa ametua Nou Camp.
 
Hivyo, ndivyo mastaa wa maana kwenye soka walivyochangia mikwanja mrefu kwenye soko la usajili, ambapo straika Romelu Lukaku akiingia kwenye orodha kwa saini zake kugharimu Euro 140.2 milioni alipohama kutoka Anderlecht, Chelsea, West Brom, Everton na sasa Man United.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…