Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Koscielny ameitisha mgomo huko Arsenal akitaka afunguliwe mlango wa kutokea, huku klabu za tatu za Ufaransa Bordeaux, Lyon na Rennes zikionyesha dhamira ya dhati ya kunasa huduma ya beki huyo wa kati mwenye umri wa miaka 33. Pia Barcelona inahusishwa na mpango wa kumnasa akazibe pengo la Samuel Umtiti endapo ataondoka katika dili la kubadilishana wachezaji na PSG ili Neymar atue Camp Nou. Koscielny amebakiza mkataba wa mwaka mmoja kwenye kikosi hicho na hivyo anataka Arsenal wamwachie aondoke bure.
 
Shida ni kwamba Arsenal wanahitaji kupata Pauni 10 milioni kwenye mauzo ya beki huyo, kwamba hawapo tayari kumwacha tu aondoke kitu ambacho kimewaingiza vitani na mchezaji wao Koscielny.

Ripoti zinadai kwamba beki huyo yupo tayari hata kuununua mkataba wake, ambao analipwa Pauni 90,000 kwa wiki ili tu aachane na Arsenal. Itakuwaje, Koscielny ataondoka kwa mgomo wake huo au Arsenal watakaza na kugoma kumwachia?

Hata hivyo, Koscielny si mchezaji wa kwanza staa kwenye Ligi Kuu England kuingia kwenye mgomo wa kushinikiza auzwe na klabu yake.
 
Riyad Mahrez

(Leicester City)

Staa wa Leicester City, Riyad Mahrez aliingia kwenye mgomo baada ya uhamisho wake wa kwenda Manchester City kugomewa.

Kilichotokea ni kwamba Mahrez aliingia kwenye mgomo kwa wiki mbili na kukosa mechi ya kwanza ya msimu mpya baada ya Leicester City kugoma kumuuza kwenda Man City. Hilo lilitokea kwenye dirisha la Januari mwaka jana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…