Maisha ni kuchagua! Maisha sio kutafuta, Ukitafuta maisha bila kuchagua mwisho wa siku ni kushindwa kufikia malengo, Chagua maisha upendayo kuyaishi ili uweze kuwa na uthubutu hata kufikia uchaguzi wako, Maana IMANI ni kutarajia na uwapo na IMANI na kile ulichochagua MUNGU husimamia hicho, Usiyatafute maisha kwani mwisho wake ni kutenda mabaya... ASUBUHI NJEMA.
Mwanamke nalijuwa hitaji lako kwa Mwanaume, Kwamba unalilia UPENDO lakini kwa sura ya mapenzi ya sasa UBINAFSI umetangulia mbele na UPENDO ukawa nyuma yake, Kwamba walio wengi wanajaribu kuliko KUMAANISHA.