Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Gharama za uhifadhi wa simba ni kubwa sana, inajumlisha gharama za uhifadhi wa mazingira yake asilia, gharama za kuhifadhi wanyama ambao wanaliwa na simba ambao ndio chakula cha simba, gharama za utafiti na ufuatiliaji wake, gharama za kuzuia madhara mabaya kama vile mioto isiyokusudiwa, magonjwa na gharama za kuajiri maaskari kwa ajili ya doria na uhifadhi kwa ujumla.
 
Kwa utafiti ulofanyika maeneo mengi ya Afrika unaonyesha gharama za uhifadhi kwa kilomita moja ya mraba kwa mwaka ni dola 500 sasa hi dola 500 ni ka kilomita za mraba moja tu, sasa chukulia hifadhi ina kilomita za mraba 20,000 au 14,000. Kwa ukubwa huo wa hifadhi zetu, na unakuta nchi kama Tanzania ina maeneo mengi sana makubwa kwa ajili ya uhifadhi wa wanyamapori, kwa kweli sio gharama ndogo hata kidogo.
 
Sasa tuje kwa simba, simba anaweza kuishi hadi zaidi ya miaka 12, na simba ana uwezo wa kutembea kwa siku zaidi ya kilometa 6, ukichukua kilomita hizo zidisha kwa mwezi na mwaka na mwaka na pia zidisha kwa umri anaoweza kuishi utapata ni mamilioni ya shilingi. Sasa chukulia huyo simba ametembea kilomita 500 kwa mwaka zidisha na gharama ya kila kilomita halafu zidisha tena kwa umri wake utapata mamilioni ya dola. Sasa huyo ni simba mmoja
 
Gharama hizo ni kwa nchi nyingi za Afrika, sasa kwa nchi za wenzetu kama Marekani gharama za uhifadhi wa simba mmoja kwa kilomita moja ya mraba n idola 2,000 sasa zidisha hizo hela kwa kilomita alizotembea simba huyo ndani ya hifadhi kwa mwaka, halafu uzidishe na umri wasimba huyo hadi anafikia wakati wa kuuwawa, utapata ni mamilioni ya dola.
 
Mfano mzuri ni kifo cha simba maarufu sana aliyeuwawa mwezi June mwaka 2015 katika hifadhi ya taifa ya Hwange nchini Zimbabwe, simba huyo alijulikana kwa jina la Cecil. Simba huyu alikuwa amefungwa kola na alikuwa anafuatiliwa mienendo yake na watafiti wa mradi wa utafiti wa simba katika hifadhi ya Hwange. Cecil aliuwawa kimakoosa na muwindaji aliyejulikana kwa jina la Walter Palmer ambaye ni daktari wa meno lakini pia ni mwindaji tajiri sana.
 
Walter alifanya makosa makubwa sana kwa kumuua Cecil ambaye alikuwa kipenzi cha watalii na wageni wengi waliotembelea hifadhi ya Hwange. Tafiti zinaonyesha Cecili alipigwa picha zadi ya laki moja na wageni, hata wanakijiji walimfahamu sana simba huyu, hivyo walimpenda na akawa kivutio kikubwa sana katika hifadhi hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…