Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

HAYA NDIO MAISHA

[emoji871]Mtu akitaka kupika MAHARAGE, lazima ayachambue. Wakati wa kuchambua yale yanayoonekana kwa macho ni MABOVU hutupwa na Yale yanayoonekana MAZIMA, hupikwa na kuliwa.

Lakini cha kushangaza, hayo mengine yaliyoonekana ni MABOVU, Mvua ikinyesha huota na kuchanua mpaka unaweza kusikia mama akimwambia mototo, "Ng'oa tu hayo majani lakini maharage yaliyochanua na kupendeza yawekee udongo ili yachanue zaidi".

Vivyo hivyo katika maisha, Watu wanaweza wasione thamani yako kulingana na hali na mwonekano wako wa sasa na mazingira yanayokuzunguka. Watu wanaweza wakakubagua, wakakutenga na kukudharau kwa kukuona hufai kwa kuangalia hali uliyonayo kwa sasa.

BROTHER & SISTERS , hutakiwi kubishana nao. Kaa kimya, Baraka zako zikianza kukujia watakuona jinsi unavyochanua na kupendeza kama maharage Yale yaliyotupwa kisa ni mabovu.

Tuthamini UTU wa watu bila kujali HALI zao kimaisha, RANGI zao, DINI zao, MAKABILA yao, ITIKADI zao, n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…