Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FAHAMU KUHUSU MWEZI WA DUNIA
(THE EARTH'S MOON)
1. JE MWEZI NI NINI?
Wengi tunaufahamu mwezi kwa kuuona angani ukielea, na tunaweza kuuona kipindi fulani mchana ama jioni lakini mwezi huonekana vizuri zaidi wakati wa Usiku. Lakini je, tumeshawahi kujiuluza kitu tunachokiona ni nini? Nitajaribu kugusia mambo machache yatakayokupa mwanga juu ya ukweli kuhusu MWEZI.
 
Mwezi huu unajulikana kama Mwezi wa Dunia. (The Earth's Moon).
MWEZI ni kitu kikubwa cha ajabu kinachoelea angani na chenye uhusiano wa karibu na dunia, wataalam wa anga hukiita kitu hicho SETILAITI YA ASILI (Natural Satellite). Mwezi sio nyota wala mwezi sio Sayari.
 
2.MWEZI UNA UKUBWA GANI?
Mwezi sio mkubwa kama sayari ya Dunia, Eneo la ukubwa wa mwezi ni asilimia 27% tu ya ukubwa wa eneo la dunia, ni sawa na kusema ukubwa wa mwezi unakaribiana na ukubwa wa bara la Asia japo bara la asia nalo pia ni kubwa kidogo kuliko eneo la mwezi.
 
AU tunaweza sema kama dunia ingekua na ukubwa sawa na Sarafu ya shilingi 500 basi Mwezi ungelingana na ukubwa wa punje ndogo ya maharage. Uzito wa Duni mara 81 zaidi ya uzito wa mwezi.
Mwezini hakuna madini ya chuma wala mwezini hakuna kabisa maji.
 
JE MWEZI ULITOKEA WAPI AU ILIKUWAJE UKAWEPO SEHEMU ULIPO SASA?
Wanasayansi walikuna vichwa sana katika kutafuta majibu ya maswali mengi yaliyoulizwa kuhusu chanzo cha mwezi. Japo kuna nadharia mbalimbali (Nne zinazofahamika kwa mujibu wa Shirika la Anga za Juu la Marekani -NASA) zinazojaribu kuelezea chanzo cha mwezi.
 
Nadharia hizo ni
(a) FISSION THEORY
(b) CAPTURE THEORY
(c) CONDENSATION THEORY
(d) GIANT IMPACTOR
Nadharia zote hizi zinajaribu kuelezea namna mwezi ulivyotokea na mpaka ukawepo sehemu ulipo sasa, lakini katika nadharia tatu za mwanzo ilionekana bado zina madhaifu na zinaendelea kuibua maswali badala ya kujibu maswali.
 
Ndipo ilipoibuka Nadharia hii ya mwisho ya GIANT IMPACTOR ambayo ndiyo hasa ilikuja kujibu maswali mengi juu ya asili ya mwezi na hii iliibuka katikati ya miaka ya 70 baada ya wanasayansi kutuma vyombo vya anga kwenda mwezini na kuleta udongo wa mwezini uliotumika katika utafiti wa kujua chanzo chake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…