Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kipindi cha pili, Man United iliingia uwanjani ikiwa na shauku ya kupata mabao mengine zaidi ambapo, Rashford na Anthony Martial waliongoza mashambulizi huku Pogba akisimama eneo la katikati akishrikiana na Andres Perreira wakati safu ya ulinzi ilikuwa chini ya beki mpya wa kati, Harry Maguire akicheza sambamba na Wan Bissaka, Victor Linderlof na Luke Shaw walimfanya Dea Gea kuwa salama muda wote.
 
Katika mchezo huo, Man United iliandika bao la pili dakika ya 65 kupitia kwa Martial akiunganisha krosi ya Perreira kabla ya Rashford tena kupachika bao la tatu. Iliwachukua Man United sekunde 95 tu kufunga mabao mawili la pili na la tatu.
 
Kama vile ikionekana kuwa matokeo yanakwenda kubaki 3-0, dakika ya 82 ya mchezo kinda mpya wa Man United, Daniel James aliyeingia kuchukua nafasi ya Perreira alipigilia msumari wa mwisho kwa kupachika bao 4-0 akitumia vyema pasi ya Pogba, ambaye kwenye mchezo huo alipiga pasi mbili za mabao.
 
Takwimu za mwisho wa mchezo zimeonyesha kwamba, Chelsea ilikuwa na umiliki wa mpira kwa asilimia 53.8 dhidi ya 46.2 za Man United huku ikipiga mashuti 18 na saba kati ya hayo ndio yalilenga lango wakati kwa upande wa wapinzani wao, walipiga mashuti 11 huku matano yakilenga goli.
Chelsea ilipata kona tano dhidi ya tatu za Man United.
 
VIKOSI:
Manchester United: De Gea; Wan-Bissaka, Maguire, Lindelof, Shaw; McTominay, Pogba; Pereira (James), Lingard (Mata), Martial; Rashford (Greenwood)
Chelsea: Arrizabalaga; Azpilicueta, Christensen, Zouma, Emerson Palmieri; Jorginho, Kovacic (Kante); Pedro, Barkley (Pulisic), Mount; Abraham (Giroud).
 
Lakini, tangu Ferguson ameondoka Old Trafford baada ya kustaafu soka, makocha waliofuatia wamefanya uamuzi mbalimbali ikiwemo kuwauza ama kutowapa nafasi wachezaji ambao waliachwa na mkongwe huyo.

Hawa hapa wachezaji wa mwisho kusajiliwa na Ferguson katika kikosi cha Manchester United, lakini baadaye wakaufuata mlango wa kutokea ulipo.
 
Freddie Veseli

Mwaka 2012, Ferguson alivuka mpaka na kuingia kwenye ngome ya Manchester City na kumbeba beki huyu mwenye asili ya Uswisi. Veseli alitua Man United akiwa ametoka kuipa zawadi ya ubingwa wa dunia Uswisi kwa wachezaji chini ya miaka 17.
 
Mwaka 2016 aliitwa kuichezea Uswisi dhidi Ufaransa kwenye michuano ya Euro.

Shinji Kagawa

Baada ya kumkosa Eden Hazard ambaye alikuwa na uhakika wa kumnasa Juni 22, mwaka 2012, Ferguson alivamia Borrusia Dotmund na kumsajili winga wa Kijapani, Kagawa huku Man United wakitoa Pauni 12 milioni.

Chini ya Ferguson, Kagawa alishinda ubingwa wa Ligi Kuu England huku akifunga mabao sita na kuchangia mengine nane kwenye mechi 38 alizocheza.

Ferguson alipoondoka, mrithi wake David Moyes hakuendelea naye na akamuweka sokoni na Kagwa akarudi zake Dortmund
 
Nick Powell

Powell alijiunga na Manchester United, Julai 2, mwaka 2012 akitokea Crewe Alexandra, katika dili linalodaiwa kuigharimu United pauni 6 milioni. Aliingia dimbani mara tisa katika misimu minne aliyokaa Old Trafford na kufunga bao moja tofauti na ilivyotarajiwa.

Akapelekwa kwa mkopo Hull, Leicester na Wigan kabla ya kuamua kutua Wigan bure (2016). Akiwa hapo, Powell amekuwa mchezaji wa kutegemewa, ambapo aliwasaidia kupanda daraja. Inadaiwa kuwa, Wigan wamekataa ofa ya Pauni 5 milioni kutoka Brighton.
 
Robin Van Persie

Alinunuliwa kwa sababu maalumu na alipozifanikisha akaondoka kwa sababu maalumu. Ndio, Ferguson mwishoni mwa utawala wake aliwaumiza mashabiki wa Arsenal kwa kumnunua nahodha na mpachika mabao wao Robin Van Persie na kumpeleka Old Traofford.

Pauni 24, milioni zilitosha kuwatia hasira Arsenal, ambapo msimu wake wa kwanza tu akaipa United taji na kuwa Mfungaji Bora akifunga mabao 30.
 
Hata hivyo, mambo yalibadilika baada ya kuingia Moyes na baadaye Louis Van Gaal ambaye aliishia kumuuza tena kwa dau dogo tu staa huyo kutokana na kasi yake ya kufumania nyavu kushuka.

Alitua Fernabahce kwa dau la pauni 3.8 milioni na kufunga mabao 16 kisha akatimkia zake Feyenoord mwaka 2017 na kuipa ubingwa wa KNVP.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…