Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Salah amekuwa mmoja wa vinara wa mabao kwenye Ligi Kuu England tangu alipojiunga na Liverpool mwaka 2017, akishinda Kiatu cha Dhahabu kwa misimu yote miwili iliyopita, akifunga mabao 72 katika mechi 107 alizocheza kwenye michuano yote.
 
Kwa mujibu wa The Sun, Real Madrid wameonyesha dhamira ya dhati ya kuhitaji saini ya mshambuliaji huyo na walitaka kumnasa kwenye majira haya ya kiangazi kabla ya kuamua kuliweka kando jambo hilo wakisubiri dirisha la majira ya kiangazi la mwakani.
 
Kwa mujibu wa Daily Mail, Sancho ataigharimu timu itakayohitaji saini yake zaidi ya Pauni 100 milioni. Man United walihitaji huduma ya winga huyo wa Kingereza na walijaribu kufanya hivyo kwenye dirisha la kiangazi huko Ulaya kabla halijafungwa upande wa England.
 
Man City nao wamekuwa wakimfuatilia kwa karibu mchezaji huyo aliyewahi kuwa kwenye kikosi chao kabla ya kumpiga bei kwenda Dortmund kwa Pauni 7 milioni mwaka 2017.
 
TETESI za nahodha wa Harambee Stars Victor Wanyama kuihama Tottenham Hotspurs zimekolea huku ripoti za sasa zikiarifu kiungo huyo anahesabu magethaa tu kabla ya kuishia zake Uturuki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…