Ukiwa Dar waweza jua daladala ni ya njia ipi kwa kuangalia tu abiria wanaoshuka au kupanda.
Ukiona daladala abiria wengi wamevaa madela na baraghashia nyingi na wanaongea sana hiyo daladala ni ya kuelekea Temeke.
Ukiona wanaopanda dalada wengi wamevaa jeans na vimini hata vibibi vikiwa na vimini na vikaptula, hiyo daladala ni ya kuelekea njia ya Mikocheni, Masaki na Mwenge & Tegeta.
Ukiona daladala wengi wanaopanda ni weupe weupe na wana meno ya rangirangi kama gold ni daladala ya kwenda Kimara & maeneo Mbezi mwisho
Ukiona daladala ina watu warefu wengi na wengine wengi unawaona ni weusi sana na wote wanaonekana kama 'full time' wako serious usoni hiyo daladala ni ya kuelekea Gongolamboto.
Ukiona wanaopanda daladala wana fujo na papara, ni kama hawana uhakika wa kupata seats .. hao ni Mbagala, Kisemvule & Kisewe
Ukiona daladala jingine waliopanda wengi wafupi kwa kimo na wana sura za tabasamu tabasamu na hawana haraka.. hiyo ni daladala ya kuelekea Kigogo, Mburahati & Mabibo.
Ila ukiona daladala .. wanaoshuka wamechafuka VUMBI kila sehemu usipate taabu... hizo ni daladala za MAKONGO JUU.[emoji23][emoji23]