Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hali hiyo husababishwa na Mtu kutokunywa maji ya kutosha, Kuunguzwa na jua na joto kali vinavyofanya maji mengi kupotea, Matumizi ya vipodozi vikali vinavyoharibu ngozi na mfumo wa maisha ya ngozi, Ngozi kuzeeka, Ukosefu wa mlo kamili (bora), Kemikali zinazokausha ngozi kama vile kemikali za kusafishia sabuni za kufulia na kuoshea vyombo na Kemikali za kuua vijidudu zenye asili ya pombe (Kwa mfano Spiriti), Ngozi kutofunikwa na mafuta ya kutosha kuzuia maji yasipotee.
 
Pili ngozi kavu ni rahisi zaidi kupata maambukizi, magonjwa na majeraha. Kadiri ukavu wa ngozi unavyozidi ndivyo magonjwa yanavyokuja na kuiharibu zaidi ngozi, Pia ngozi kavu ni kwamba hunyauka na kusinyaa, na kufanya muonekano wa ngozi usiwe mzuri.
 
Kupaka mafuta ya kutosha yenye uwezo wa kuongeza maji na kutunza unyevu wa kutosha na kuifanya iwe na maji ya kutosha. Vipodozi unavyoweza kutumia hapa ni Losheni zilizoandikwa MOISTURIZER, mafuta yaliyoandikwa PETROLEUM JELLY, au Glycerine, Kunywa maji ya kutosha kila siku ili yafike na kukaa kwenye ngozi na kuitunza
 
Epuka jua na joto kali. Unaweza kufanya hivi kwa kufunika vizuri mwili wako, kupaka vipodozi vinavyoukinga mwili dhidi ya miale mikali ya jua (SUN BLOCKERS/SCREENS) , kuepuka kushinda au kufanya kazi juani, kuoga mara kwa mara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…