Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Nyie nyie Mungu huyu ana makusudi ya kutuangamiza wanaume tunao utumia vizuri uanaume wetu!!!
Niwekewe hao mbele yangu nichague mmoja, kwanini? Kwamba siwawezi kuwatemesha uji?
Kama ni kuchagua, hao wawili(mmoja anakuwa mchepuko huru) wa katikati naondoka nao wote. Ila, piga ua nikatwe mtama garagaza kwenye matope sijui kwenye vumbi, na kwenye macho nipakwe pilipili ili nisione, hao wawili wa pembeni lazima wawe michepuko wote ili nafsi itulie.
 
Utafiti unaonyesha kwamba wafanyakazi katika makampuni yenye mabosi wenye umri mdogo kuliko wao huwa na hisia hasi ikilinganishwa na wale walio na mabosi waliowazidi umri.
 
Wape Heshima Wanayostahili



Bosi wako anaweza kuwa na umri mdogo kuliko wewe, lakini hii haimaanishi kwamba hana uwezo unaotakiwa. Ni muhimu kusikiliza na kuheshimu maamuzi yao. Hii inamaanisha kwamba mambo ambayo utafanya ili kuonyesha heshima kwa bosi wako wa zamani hayana tofauti na kwa bosi mwenye umri mdogo kwako. Kubali kuwa yeye ni mtu sahihi kufanya kazi hioyo na daima kuwa muwazi kwa mawazo anayoleta na kukubali kwa mtazamo chanya. Ikiwa unaonyesha heshima kwa bosi wako, ni wazi kabisa kuwa utaipata ya kwake kwa urahisi pia.
 
Tumia Uzoefu Wako kwa Hekima

Uzoefu wako katika kufanya kazi katika kampuni hiyo ni moja ya zana muhimu zaidi ambazo unaweza kutumia katika kuimarisha uzalishaji na ufanisi wa shirika. Unaweza kutumia hii kumsaidia bosi wako mdogo kukuza ujuzi wake katika kuongoza timu na kusaidia kampuni kukua. Bosi wako anaweza kuwa na ujuzi katika eneo fulani kama vile teknolojia lakini hajui mengi kuhusu mawasiliano. Unapaswa kuwa tayari kumfundisha ujuzi uliyopata kwa miaka mingi na atatambua mchango wako kwa kampuni kirahisi zaidi kwa ukuaji bora wa kazi yako baadaye
 
Kuwa Tayari Kubadilika na Kujifunza



Kuwa tayari kubadilika kuhusu namna mambo yanavyofanyika katika ofisi ni muhimu. Bosi wako anaweza kuchagua njia tofauti ya kutatua matatizo katika kampuni. Kizazi cha vijana kinasemekana kupenda teknolojia zaidi kufanyia kazi, hivyo unaweza kuhitaji kubadilika na kujifunza ufanane na kasi ya bosi wako. Makampuni mengine hufanya kazi na watu katika sehemu mbalimbali za ulimwengu. Kwa hivyo bosi wako anaweza kuchagua mitandao kama vile Slack kwa mawasiliano. Daima kuwa tayari kukubali changamoto mpya kama hizi.
 
Usiumize Kichwa Sana

Kazi na maamuzi uliyofanya katika kazi zako ndio yamekusaidia uwe katika nafasi yako ya sasa. Uko katika nafasi hii kwa sababu ya kazi yako na kwamba unapaswa kujivunia. Hutakiwi kufikiri kwamba timu ya uongozi inakuona kuwa duni zaidi kwa sababu walitoa jukumu la ubosi kwa mtu mwingine aliye mdogo kuliko wewe. Kuwa na ujasiri kukubaliana na ukweli kwamba walikuajiri ili kuleta thamani maalum kwa timu. Hakikisha unajaribu kufanya kazi na bosi wako mdogo na kujitoa kwa kila ulicho nacho kufanikisha kazi hiyo.
 
Mawasiliano ni Muhimu



Mawasiliano ya wazi kati ya wewe na bosi wako yatawafanya muweze kuelewana na kujenga mazingira mazuri ya kazi. Tafuta njia yake nzuri ya mawasiliano ili kuunda mazungumzo sahihi, kujenga imani na kuboresha tija ya kampuni.
 
Zingatia Ukuaji wako wa Kazi na Kampuni

Mwisho, unapaswa kukumbuka kuwa upo katika nafasi uliyopo kama ulivyokusudia waukianza kazi yako. Daima amini kwamba kazi yako itaendelea kukua bila kujali tofauti ya umri kati yako na bosi wako. Kwa kuongeza, kumbuka kwamba wewe na bosi wako mpo kwenye timu moja na lengo lenu ni moja, kukuza kampuni.
 
Kufanya mtu avutiwe nawe kwa mara ya kwanza kazini ni muhimu sana ndani ya wiki ya kwanza ya ajira yako. Inaweza kukutisha kidogo, kutokana mambo kadha wa kadha kama vile shinikizo la kukutana na watu wapya, kuwa na hisia zilizo katikati, kuelewa mazingira mapya ya kazi na kadhalika. Kibinadamu, hisia hizi ni za kawaida kabisa. Hupaswi kuwa na wasiwasi juu ya kukutana kwa wafanyakazi au viongozi wako.
Hivi ni vidokezo vya vitu vya kufanya ili kuwa imara katika wiki yako ya kwanza kwenye kazi yako mpya.
 
Zingatia na Elewa Mfumo na Tamaduni Zao



Kuzingatia kwa makini mtindo wa mawasiliano na tamaduni miongoni mwa wafanyakazi wenzako ni mwanzo mzuri wa kukabiliana na kazi yako mpya. Ni muhimu kuelewa mwingiliano baina ya wafanyakazi wenzako, ni nani utakayemfata wakati una maswali na ni muhimu kujua majina ya watu ambao utakutana nao. Hakikisha unasoma nyaraka na kuwa unatambua na kuandika pembeni kila kitu muhimu unachojifunza.
 
Jipange

Wiki ya kwanza pia ni wakati mzuri wa kuhakikisha utambua vitu muhimu ambavyo vinasaidia mtiririko wako wa kazi. Anza kwa kuandaa meza yako, saini yako ya barua pepe, akaunti za mitandao ya kijamii na hakikisha una mawasiliano ya watu wote muhimu ofisini. Pia, hakikisha unafahamu maeneo muhimu kama vile sehemu za kupumzikia, eneo la chakula cha mchana na huduma zingine zinazopatikana ndani ya ofisi yenu. Zaidi ya hayo, hakikisha unapima safari yako ili ujue muda sahihi wa kuondoka nyumbani na njia za usafiri utakayotumia ili kuepuka kuchelewa kazini.
 
Jenga Mahusiano



Kuwa na mahusiano na wafanyakazi wenzako kutasaidia kuwa na ujasiri utakapoanza kazi yako mpya. Tafuta muda sahihi utoe utambulisho mfupi na waharaka kwa watu wapya ambao unakutana nao. Unaweza usipate rafiki wako wa kudumu hapo, lakini ukapata mtu ambaye mnaweza kuendana na akakupa utulivu utakaohitajika. Ni muhimu kuwa na marafiki katika hatua hii ili kukusaidia katika kuwa ujasiri na utendaji mzuri kazini. Tafiti iliochapishwa katika jarida la Journal of Business and Psychology unaonyesha kwamba urafiki mahali pa kazi una faida za moja kwa moja kwa wafanyakazi na utendaji kazi, kuridhika kufanya kazi hiyo pamoja na faida ya moja kwa moja juu ya kujitolea katika shirika.
 
Uliza Maswali Mengi Iwezekanavyo

Ili kujifunza haraka katika mazingira yako mapya ya kazi, utahitajika kuwasiliana na viongozi wako na wafanyakazi wenzako mara nyingi iwezekanavyo. Tenga kabisa mambo muhimu unayohitaji kujua, kama swali, ushauri au kuruhusiwa kufanya kitu fulani na uliza kwa wakati fulani bila kupoteza muda. Kumbuka kuandika maswali yako ili usisahau na kuuliza yote pamoja ili kuepuka nenda rudi. Pia, unaweza kutafuta majibu ya maswali yako kwanza kupitia mitandao kama vile Google au Youtube kabla ya kwenda kuuliza ili kuokoa muda.
 
Toa na Kubali Msaada Wao



Onyesha nia ya kujenga uhusiano mzuri na wafanyakazi wenzako kwa kujitolea kuwasaidia katika kazi zao wakati wowote watakapohitaji. Hii itakuwezesha kujifunza na kupata ufahamu juu ya jinsi mambo yanavyofanyika. Ikiwa wataamua kukupa msaada kwa kazi unayofanya, mara zote pokea msaada wao kwa mikono miwili hata kama una uwezo wa kufanya kazi hiyo yote mwenyewe. Hii itaunda uhusiano bora kati yako na wao na uwezekano wa kujifunza njia rahisi ya kukamilisha kazi zako.
 
Weka Malengo na Mjulishe Bosi Wako

Mwisho, wiki yako ya kwanza ni wakati mzuri wa kuweka malengo na kujua nini hasa Bosi wako anataka kutoka kwako. Hii itakuwezesha kujua mwelekeo sahihi na kasi ya kufikia malengo yako. Wakati wa mikutano ya moja kwa moja na bosi wako, tumia wakati huu kumjulisha kuhusu unayojifunza, watu unaokutana nao na changamoto unazozikabili. Pia hakikisha kwamba unaelewa malengo yako na jinsi ufanisi wa kazi zako unavyopimwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…