Katika kitabu chake, 'Per Mertesacker: Big Friendly German', beki huyo aliandika: "Tulipopoteza mechi, basi tuliendelea kupoteza nyingine mfululizo zilizofuatia. Tungeweza kuonyesha ubora wetu kwenye mechi sita za Kombe la FA, lakini kwenye mechi 38 za Ligi Kuu England za kucheza kwa miezi 10 tulikuwa watu wengine kabisa.
Tulishindwa kuwa na ule mwendelezo wa ushindi kama timu kubwa. Huwezi kushinda ubingwa wa ligi kama unapoteza mechi nane ndani ya msimu. “Kocha Arsene Wenger siku zote yeye alikuwa mtu wa kuamini timu yake, hakuwahi kukosa matumaini.