Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Bila shaka umewahinkusikia mtu akisema, wach nicheke niongoze siku za kuishi. Kama umewahi kusikia nataka nikuongezee kitu ya kwamba wataalam wa saikolojia wanasema kuwa kucheka au kufurahi ni moja ya tiba kwa afya ambayo huifanya miili yetu kubaki na afya bora zaidi.
 
Husaidia kuimarisha afya ya mapafu
Unapocheka husaidia mapafu yako kutanuka na kuingiza ndani hewa ya safi yaani oxygen. Hivyo unapocheka zaidi tambua kuwa unasaidia kiwango cha hewa kuingia cha kutosha ndani ya mwili na kusaidia damu kusambaa vyema mwilini.
 
Husaidia kuboresha utendaji kazi wa moyo
Kitendo cha kucheka au kufurahi husaidia kukuweka mbali dhidi ya shinikizo la damu la kushuka, kwa sababu husaidia kuongeza mzunguko wa damu mwilini na pia kusaidia mishipa ya damu kutenda kazi vizuri.
 
Watu wanaugua maradhi mbalimbali, lakini wengi wao hawapendi kwenda hospitali kufanya vipimo au kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa daktari, hii inaweza kuchangiwa kwa kiasi kikubwa na gharama zitokanazo mara tu mtu anapoamua kwenda hospitali kumuona daktari kwa ajili ya kumueleza mabadiliko anayoyasikia mwilini mwake yanayompelekea kujisikia hali isiyo ya kawaida.
 
Ijapokuwa haishauriwi kuhisi unaumwa ugonjwa fulani ilihali mara ya mwisho ulijisikia hivyo na kukutwa na homa iyo unayodhani pengine imejirudia, kiafya na kitaalamu inashauriwa kupimwa kwanza afya ili kubaini nini hasa chanzo cha mabadiliko ya mwili wako, na si vyema kuhisi na kuanza kutibu ugonjwa unaohisi unaumwa, wengi wamekuwa na tabia hiyo.
 
Huweza kusababbisha kifo.

Ifahamike kuwa dawa ni sumu zinazokabili vimelea vya magonjwa. Hivyo kutumia dawa vibaya kunaweza kusababisha kifo watu wenye matatizo maalumu kama vile maradhi ya moyo pamoja na shinikizo la damu, wanapaswa kuwa makini na dawa wanazozitumia kwani zinaweza kuchochea matatizo yao na hatimaye kifo.
 
Huweza kusababisha saratani.

Dawa zinapoingia mwilini kimakosa na kushindwa kufanya kazi yake, zinaweza kuharibu baadhi ya seli za mwili na kuzifanya kugeuka seli za saratani. Hivyo hakikisha dawa unayoitumia ni sahihi na inalenga ugonjwa husika.
 
Husababisha usugu wa maradhi

Mtaalamu wa afya hukupa kiwango (dosage) cha dawa kulingana na vipimo alivyovifanya; hivyo kutumia dawa bila vipimo vya kitaalamu kunaweza kusababisha vimelea vya ugonjwa vizoee dawa husika na kusababisha ugonjwa huo usitibike tena, hili ndilo linalosababisha maradhi kama vile malaria sugu au UTI sugu. Hivyo kabla ya kutumia dawa ni vyema ukafanya uchunguzi wa kitaalamu
 
Huongeza sumu mwilini.

Dawa zimetengenezwa kwa kutumia kemikali mbalimbali ambazo kimsingi ni sumu zinazoua vimelea vya magonjwa, hivyo kutumia dawa bila vipimo kunasababishia kuongeza sumu za dawa hizo mwilini mwako kwani umetumia dawa ambazo mwili hauzihitaji kukabili ugonjwa husika na sumu hizi zinapokusanyika mwilini zinaweza kuleta athari mbalimbali za muda mfupi au hata mrefu.
 
Hivyo ni muhimu ikumbuke kuwa dalili za ugonjwa mmoja zinaweza kuwa dalili za ugonjwa mwingine pia. Hivyo ni muhimu kufanya uchunguzi pamoja na kutafuta ushauri wa kitabibu kabla ya kutumia dawa zozote kutibu maradhi yanayokukabili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…