Ni mapema sana bado na pengine atabadili mambo, lakini hakika sijaona ninachotarajia kukiona kutoka kwake.”
Wakati akikosoa mchango wa Pepe, Keown amevutiwa na kiwango cha mgeni mwenzake Pepe, Kieran Tierney, 22.
Beki huyo wa kushoto wa kimataifa wa Scotland ameingia kirahisi kikosini baada ya kutua akitokea Celtic akiwa majeruhi, lakini sasa ametumia mechi mbili tu kuthibitisha anamweka Sead Kolasinac katika presha ya kuwania namba hiyo.
Katika mechi hiyo, Tierney alitoa pasi ya bao kwa Dani Ceballos dakika ya 57 huku mabao mengine yalifungwa na kinda Mbrazili, Gabriel Martinelli dakika ya 13 na 16 na jingine Joe Willock dakika ya 22.