Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kundi la watu wenye umri wa miaka 40 hadi 44, kiwango cha shinikizo la damu kwa wanaume ni asilimia 6.4 na wanawake 11.5. Wakati kundi la watu wenye umri wa miaka 30 hadi 34, kiwango cha shinikio la damu ni asilimia 6.4 wanaume na wanawake ni asilimia 5.9. Maendeleo ya utafiti wa miti ya habiscus sabdariff umekuja wakati muafaka ambako dawa za mitishamba zinapata umaarufu nchini mwetu kutokana na juhudi za watafiti mbalimbali walioamua kuinua kiwango cha dawa za mitishamba nchini.
 
Mti huo unapatikana Tanzania na unapandwa mkoani Kilimanjaro, Morogoro, Dodoma na Pwani. Taasisi ya Dawa za Mitishamba katika Chuo Kikuu cha Sayansi ya Afya Muhimbili (MUCHS), inaitambulisha dawa hiyo kama chanzo cha kuleta lishe bora na kinywaji chenye kuleta afya.
Kinachotakiwa ni kuchukua maganda ya miti hiyo na kuchanganya na maji, halafu tikisa na utapata kinywaji kizuri cha kuburudisha. Mti huu ni miongoni mwa mimea ambayo ipo kwenye mradi wa kutaka liwe zao la kuzalishwa katika maeneo mengi ili liwe chanzo cha mapato kwa wakazi wa Kongowe, mkoani Pwani.
 
Mpango wa muda mrefu wa zao hilo ni kupanga daraja la uwezo wa zao, ama kutibu peke yake au kwa kuunganisha na dawa nyingine,” anasema Dk. Mainen Moshi, kiongozi wa mradi na Mkurugenzi wa Taasisi ya Mitishamba, Muhimbili. Mradi huo una malengo mawili, kwanza, una lengo la kuchangia katika mkakati wa kitaifa wa kupunguza umaskini kwa kuzalisha zao hilo na kuwa chanzo cha lishe bora na kuongeza kipato cha wananchi.
Pili, ni kuchangia katika uboreshaji sera za taifa za chakula na lishe bora ambazo zinalenga katika kuongeza mazingira ya uzalishaji lishe bora miongoni mwa watoto na wanawake hata wanaoishi na virusi vya ukimwi.
Kuwapo kwa mmea huo nchini, ni kitu kizuri na cha kujivunia, na hivi karibuni, wanasayansi wamekuwa wakiutangaza kwa nguvu zao zote, kuhakikisha taifa linatambua umuhimu wa mti huo na namna linavyoweza kuutumia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…