Manchester United wanapanga kumsajili kiungo Francisco Sebastian Cordova, ambaye anachezea klabu ya America ya Ligi Kuu nchini Mexico. Kiungo huyo mwenye miaka 22 ambaye ameichezea timu ya taifa lake kwa mara ya kwanza juma lililopita pia anatakiwa na Sevilla na Benfica. (Mail)
Mchezaji mmoja mwandamizi wa Manchester United aliandaa mlo katika moja ya mgahawa kwa kikosi kizima lakini ni wachezaji watano tu ndio waliokwenda.. (ESPN)
Juventus na Napoli wanamnyemelea mshambuliaji kinda wa klabu ya Red Bull Salzburg na timu ya taifa ya Norway striker Erling Haaland, 19, ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa vilabu vya Nottingham Forest, Leeds na Manchester City Alf-Inge Haaland. (Corriere dello Sport - in Italian)
Kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger anaamini Bayern Munich "walimlaghai" mshambuliaji wa Ujerumani Serge Gnabry, 24, ili kuihama Arsenal mwaka 2016. (Goal.com)
Mlinzi wa England Harry Maguire, 26, anaamini usajili wake wa pauni milioni 80 ulikuwa ni "dili nzuri" baina ya vilabu vya Manchester United na Leicester. (Leicester Mercury)
Kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino napanga kuwauza wachezaji kadhaa wa klabu hiyo baada ya kuanza msimu kwa kiwango kibovu. Wachezaji watakaowekwa sokoni mwezi Januari ni; Eric Dier, 25, Christian Eriksen, 27, Serge Aurier, 26, Victor Wanyama, 28, pamoja na Danny Rose, 29. (Times - subscription required)
Borussia Dortmund wameungana na Arsenal, Juventus na Paris St-Germain katika kufuatilia maendeleo ya winga kinda wa Celtic ya Uskochi, Karamoko Dembele, mwenye miaka 16. (Bild - in German)
Kocha David Moyes yupo tayari kurudi kuifunza klabu yake ya zamani ya Everton, katika kipindi ambaco kocha wa sasa Marco Silva akiwa katika shinikizo kubwa baada ya timu hiyo kuwa chini ya mstari wa kushuka daraja. (Mirror)
Crystal Palace watalazimika kulipa pauni milioni ili 22 wamsajili mshambuliaji wa Chelsea na timu ya taifa ya Ubelgiji Michy Batshuayi, 26, ambaye yupo kwa mkopo Palace toka Januari mwaka huu. (Express