Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Miamba hiyo ya Hispania, inaoyoongoza msimamo wa La Liga kwa sasa, mpango wao ni kuboresha safu yao ya kiungo kwenye dirisha hili la majira ya baridi, lakini shida bado hakuna makubaliano ya mwisho, yupo wa kunaswa kati ya Pogba au Eriksen.
 
Mastaa wote hao wawili wamekuwa wakihusishwa na mpango wa kutua huko Bernabeu, lakini Madrid ilishindwa kunasa huduma zao baada ya kutumia karibu Pauni 275 milioni kwa usajili wa wachezaji Eden Hazard, Eder Militao, Ferland Mendy na Luka Jovic.
 
Kwa mujibu wa ripoti za kutoka Hispania, Perez anaamini Pauni 26.5 milioni zitatosha kumsainisha Eriksen ili atue kwenye kikosi chao Januari, lakini shida ni kwamba Zidane anataka Pogba asajiliwe kwanza na hapo ndipo linapokuja suala la kutokubaliana juu ya wakali hao wawili.
 
Zidane anamhitaji Pogba kwa haraka kwenye kikosi chake, lakini Manchester United wao wamekuwa wakisisitiza kwamba staa huyo wa Ufaransa atauzwa kwa ada inayoanzia Pauni 150 milioni kitu ambacho Perez hawezi kukifanya kwenye dirisha hilo la Januari, huku Man United wenyewe wakionekana wazi kwamba hawatakubali kuachana na silaha yao katikati ya msimu hata kama watataka kumwondoa kwenye kikosi chao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…