Anaandika Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
_________________
Uliishi, unaishi, utaishi, Kambarage. Baba wa Taifa. Uliacha Taifa, sasa tuna nchi. Uliongoza kutokea nyuma, katikati na mbele yetu.
Ulikosoa, ulikosolewa, ulijikosoa. Ulikosoa chama chako, ulikosoa serikali yako, ulijikosoa mwenyewe. Ulikosoa kanisa, ukakosoa misikiti na ukakosoa wasio na dini. Ulikosoa matajiri, ukakosoa maskini. Uliwapenda maskini bila kuutukuza umaskini.
Sitakulinganisha na yeyote, nitakutumia daima kuwamulika wengine na kujimulika.
Mwenge uliowasha, haupo mlimani kilimanjaro wala barabarani. Umo mioyoni mwa watanzania wapenda umoja, haki na amani ya kweli.
Mwalimu usife kabla sijafa.!