Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tathimini upya marafiki zako

Kila mtu ana marafiki katika maisha yake, lakini si wote wana manufaa kwako. Je ulishawahi kujiuliza ni marafiki wangapi uliokuwa nao shule ya msingi au sekondari na bado wanakufaa hadi sasa? Marafiki wanatakiwa wakuinue unapoanguka au unapozama wakuokoe na si kukuzamisha zaidi.
 
Je ni marafiki gani wa kuwaepuka?

Marafiki wasiojali muda na wavivu.
Marafiki wanopenda starehe na anasa.
Marafiki wasiopenda elimu na maarifa.
Marafiki wasiokuwa na malengo na maono ya mbeleni.
Marafiki wasiojua kuweka akiba – wao hutumia kila wanachokipata.
Marafiki wasioweza wala kupenda kukushauri na kushauriwa.
Ukiwaepuka hawa hakika utabakia na wale ambao hawatakuwa ni kikwazo kwako wewe kutimiza na kuishi ndoto zako.
 
Faida za kuoa au kuolewa na mtu sahihi:

Atakujali na kukutia moyo kila wakati.
Mtapanga mipango mabali mbali ya maendeleo pamoja.
Mtasaidiana na kutiana moyo wakati wa shida.
Mtahamasishana ili kuhakikisha manafikia ndoto zenu.
Atakusaidia kutimiza majukumu na mipango mbalimbali.
Ikiwa basi hukupata mtu stahiki katika ndoa, faida hizo hapo juu zitakuwa kinyume chake na mtokeo yake utakosa furaha na kuishi masha ya mahangaiko ambayo katu hutofikia ndoto zako
 
Jikite kwenye ratiba ya mafanikio

Tuna mambo mengi sana ya kufanya humu duniani, lakini siyo yote hutuwewezesha kutimiza ndoto zetu. Hakikisha unapanga ratiba yako kwa kuhakikisha unaongeza maarifa na unafanya kitu chochote kwa siku ili kufikia au kutimiza ndoto zako.
 
Mambo ya kuzingatia katika hili:

Tumia muda vyema (Epuka vitu vinavyopoteza muda kama vile facebook, Televisheni n.k).
Jifunze kitu kipya kila siku, pia soma vitabu na makala mbalimbali kama hii unayoisoma.
Sogeza hatua moja kila siku kuelekea malengo yako.
Weka akiba.
Linda afya yako (kwa mazoezi, tabia njema na lishe bora).
 
Tafuta muda wa kupumzika na kuburudika

Kwa kuwa unatafuta kuishi ndoto zako, haimaanishi hauhitaji kupumzika au kuburudika. Unapopumzika unaupa mwili na ubongo wako nafasi ya kuwa katika hali nzuri zaidi ili uweze kufanya kazi kwa ubora zaidi.

Kwa mfano kama unapenda piano unaweza kupiga piano au ukaenda kutazama mandhari ya asili kama vile milima na wanyama. Kumbuka epuka starehe na anasa zisizokuwa na maana kama vile pombe na uzinzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…