Baadhi ya virutubisho vilivopo katika maziwa ya mtindi ni ‘Molybdenum’,‘Potassium’, ‘Riboflavin (vitamin B2),Iodine’,‘Phosphorus’,‘Pantothenic acid (vitamin B5) ‘Zinc’,‘Calcium’ na ‘vitamin B12’
Ni lini mara yako ya mwisho kupata maziwa mtindi? Ni vyema ukayafanya kama sehemu ya chakula chako ama baada ya chakula ama kabla ya chakula, yatakusaidia. Soma faida zake hapa.
Mbali ya faida hizo, mtindi pia umeonekana kupunguza mafuta (fat) mwilini na kwa maana hiyo una uwezo wa kupunguza unene unaotokana na mafuta mengi mwilini.kwa watu wenye mpango wa kupunguza uzito wanashauriwa kunywa mtindi mara kwa mara huku wakiendelea kufanya mazoezi mbalimbali ya kupunguza uzito.
Maziwa ya mtindi yana mchango mkubwa katika ukuaji wa misuli. Hili ni kutokana na protini zinazopatikana katika maziwa.Maziwa huzuia maumivu ya misuli pamoja na kurudisha ute ulipotea kwenye maungo ya magoti na viwiko wakati wa kazi mbalimbali.Unashauriwa kunywa maziwa ya mtindi mida ya joini baada ya kutoka katika shughuli zako za siku nzima.
Utafiti unaonesha kuwa unywaji wa mtindi mara kwa mara, hasa katika kundi la wazee umeongeza uwezo wa mwili kupambana na magonjwa mbalimbali na kuufanya mfumo wa kinga mwilini kuwa imara zaidi.
Watu ambao huwa wanaishiwa na nguvu mwilini mara kwa mara wanashauriwa kupenda kunywa maziwa ya mtindi kwani huwa na uwezo wa kuupa mwili nguvu kupitia virutubisho vya wanga vinavyopatikana katika maziwa ya mtindi.
Maziwa ya mtindi pia husaidia kupunguza kiwango cha lehemu mbaya mwilini (Low Density Lipoproteins-bad cholesterol) ambayo huweza kuongeza hatari ya matatizo kama shinikizo la damu, magonjwa ya moyo na kiharusi.Maziwa ya mtindi pia uweza kupandisha kiwango cha lehemu nzuri mwilini (High Density Lipoproteins–good cholesterol) ambayo huruhusu mwili kutengeneza vitamin D na kusaidia mwili kutengeneza baadhi ya homoni. .