Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Pia usisahau kuzifanyia steaming nywele zako kwa mwezi hata mara 2, tumia steaming products kwa ajili ya natural hair au fanya steaming ya yai ni nzuri sana kwa kurutubisha nywele za asili. Osha nywele zako na shampoo kisha koroga yai na paka kichwani kwenye ngozi, Vaa kofia ya plastic kwa dakika 45, kisha osha vizuri.
 
Kitu kingine ni kuzichana vizuri nywele zako, nywele za kiafrika ambazo hazijawekwa dawa zina asili ya kujisokota au nyingine ni kipilipili hivyo mara nyingi huwa zinafungana, hivyo wakati wa kuchana inabidi uwe mwangalifu zisikatike, tumia chanuo ambalo ni pana na hakikisha umepaka hair lotion (hair moisturizer / pink lotion) kwenye nywele na mafuta ndio uanze kuchana taratibu. Wakati wa kulala jaribu kusuka mabutu na kuvaa kofia ili nywele zisijifunge au kujisokota.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…