NIGERIA: WANAFUNZI 13 WAPOTEZA MAISHA KUFUATIA VURUGU KATI YA WANAFUNZI
-
Watu 13 wamefariki kutokana na vurugu za mapigano zilizotokea baina ya wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Kogi katika eneo la Ayingba
-
Mapigano hayo yalitokea baina ya makundi mawili ya kiimani kati ya wanafunzi hao na kutokana na vurugu hizo wanafunzi wengine wamejeruhiwa
-
Kulingana na mashuhuda wamesema vurugu hizo zilianza wiki iliyopita Ijumaa ambapo wanafunzi 9 walivamiwa katika maeneo tofauti na uvamizi umeendelea huku wengine wakikatwa kwa mapanga na viungo vya miili yao kugawanywa kikatili
-
Msemaji wa Polisi katika Jimbo la Kogi, Hakeem Busari amesema timu za usalama zimetumwa katika eneo hilo na kwamba uchunguzi kuhusiana na na tukio hilo umeanza