Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Polisi Mkoani Kilimanjaro wamesema ni kweli wamepata taarifa za Watu wasiojulikana kudaiwa kuchoma Ofisi ya Kata ya Soweto, Moshi na kuteketeza nyaraka zote muhimu zilizokuwemo ndani ya ofisi hiyo na wanafuatilia kujua undani wa tukio hilo kisha watatoa taarifa zaidi baadae.
 
Polisi Mkoani Mjini Magharibi Zanzibar wamejitosa katika sakata la Binti wa Darasa la 5 aliyepewa ujauzito na kujifungua kwa njia ya upasuaji wakiapa kumsaka na kumtia mbaroni Kijana anayetuhumiwa kumpa mimba Binti huyo.
_
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mbuzini Bikiembe Mbarouk amesema waliwahi kushtushwa na utoro wa Mwanafunzi huyo ambaye hakuhudhuria shuleni kwa zaidi ya Mwezi na nusu na siku alipofika akadai alikuwa anaumwa.
_
Mwalimu amesema walimuomba Binti aende nyumbani na arudi na Wazazi ili wakatoe maelezo lakini Wazazi walipofika wakadai Mtoto huyo kila siku alikuwa akitoka nyumbani na kuaga anakwenda shuleni, baada ya tukio hilo waliamua kwenda kumpima na wakamkuta na ujauzito ambao baadae ulipelekea kujifungua kwa upasuaji.
 
Polisi Mkoani Mara wamesema bado wanaendelea kumtafuta Juma Magige ili kujua ukweli kuhusu kifo cha Suzan Kinara Mkazi wa Kitongoji cha Kiatungwe Butiama Mkoani Mara aliyefariki Dunia muda mfupi baada ya kuugua ghafla akiwa kwa Mpenzi wake huyo Juma Magige ambapo kabla ya kufariki Juma alitoa taarifa kwa Ndugu wa Suzan kuwa Mpenzi wake anaumwa sana na hawezi kuongea .
_
Ndugu walifika kwa Juma wakiongozwa na Mtoto wa Suzan anayeitwa Robert Mwasi na alipoona Mama yake yuko hoi wakati alitoka nyumbani akiwa mzima alitoa taarifa Polisi kitendo kilichopelekea Juma kukimbia na kutokomea kusikojulikana.
_
Baadae walimchukua mgonjwa kumuwahisha Hospitali lakini akapoteza Maisha wakiwa njiani.
_
Polisi wamesema wanamtafuta Juma ili kujua ukweli juu ya kifo hicho na Mtoto bado ameendelea kusisitiza kuwa ana mashaka na kifo cha Mama yake kwakuwa kimekuwa ghafla.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…