Njia zingine za Kukusaidia Kuondokana na Tatizo la Tumbo Kujaa Gesi
Tembelea hospitali mara kwa mara kuonana na Dactari
Kutokana na kwamba tumbo kujaa gesi inaweza kuletekezwa na matatizo mengine mengi ya kiafya kama tulivosoma pale juu kuna umuhimu kufanya vipimo mara kwa mara ili kujua chanzo cha tatizo lako. Kumbuka hakuna kipimo kimoja cha kujua kinachokusumbua ni vyema kuongea na dactari wako ili akupe ushauri na vipimo stahili.
Weka ratiba ya kufanya mazoezi: Kufanya mazoezi itakusaidia kuimarisha ufanyaji kazi wa mfumo wa chakula, kurahisisha usafirishaji, na hivo kutoa sumu mwilini. Fanya mazoezi walau dakika 30 mpaka 60 kwa siku mara 3 kwa week.
Kunywa maji ya kutosha: Maji hurahisisha usagaji wa chakula na utolewaji wa choo, Hakikisha unakunywa maji kila unapopata kiu. Hakuna kipimo maalumu cha kiwango cha maji unachotakiwa kutumia unaweza kuanza na glass 6 mpaka 8 itategemea na shughuli unazofanya na mazingira unayoishi.
Mara kwa mara kumeshuhudiwa ajali mbalimbali ambazo kimsingi zinatokana na madereva kutokuzingatia kanuni muhimu katika utumiaji wa vyombo vya usafiri.
Ili kuhakikisha usalama wako pamoja na watumiaji wengine wa barabara, yapo mambo kadhaa unayopaswa kuyazingatia kabla na wakati wa kuendesha gari umbali mrefu.