Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na Sweden Zlatan Ibrahimovic, 38, yupo radhi kuhamia Everton pale Carlo Ancelotti atakapokabidhiwa rasmi klabu hiyo. (Talksport)
Kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil, 31, anatarajiwa kujiunga na klabu ya Uturuki ya Fenerbahce kwa mkopo wa miezi sita katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (Fotomac, via Football.London)
Klabu ya Bruges nchini Ubelgiji inataka Yuro milioni 30 ili kumuuza mshambuliiaji wake Emmanuel Dennis huku klabu za Leicester, Brighton ana Southampton zikiwa miongoni mwa klabu zinazomnyatia. (Foot Mercato, via Leicester Mercury)
Mshambuliaji wa Tottenham na Brazil Lucas Moura, 27, amekiri kwamba alikaribia kujiunga na klabu ya Manchester United mwaka 2012 kabla ya kuamua kujunga na PSG badala yake. (ESPN Brasil, via Mirror)
Manchester United italazimika kulipa dau la £12m kwa ajenti Mino Raiola juu ya uhamisho ili kumsajili mshambuliaji wa RB Salzburg na Norway Erling Braut Haaland, 19. (Sun)
Crystal Palace ina hamu ya kumsaini aliyekuwa mshambuliaji wa zamani wa Liverpool na Sunderland Fabio Borini, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 raia wa Itali akiwa na klabu ya AC Milan kwa sasa. (Corriere Dello Sport, via Sport Witness)