Manchester United na Paris St-Germain wanampigania beki wa kulia wa Leicester City Ricardo Pereira lakini watalazimika kusubiri hadi mwisho wa msimu huu ili kufanya makubaliano yoyote na nchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 raia wa. (Le10 Sport, via Star)
Arsenal wamehusishwa na uhamisho wa beki wa kati wa RB Leipzig Dayot Upamecano na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 anaweza kuruhusiwa kuondoka katika klabu hiyo ya Ujerumani iwapo klabu hiyo itamsaini mchezaji wa Ufaransa Tanguy Kouassi, 17, kutoka klabu ya Paris St-Germain. (Le Parisien, via Mirror)
Klabu za Burnley na Brighton zinafikiria kumsaini beki wa Hamilton Jamie Hamilton, huku klabu hiyo ya Uskochi ikitaka kulipwa dau la £1.5m kumuuza kinda huyo mwenye umri wa miaka 17.. (Mail)
Mkufunzi wa Sheffield United Chris Wilder anataka kuongeza kandarasi ya beki wa Ireland John Egan, 27, na Enda Stevens, 29, pamoja na kiungo wa kati wa England John Lundstram, 25. (Sheffield Star)
Ajenti wa kiungo wa kati wa Arsenal Xhaka nasema kwamba mchezaji huuyo mwenye umri wa miaka 27 raia wa Uswizi amekubali uhamisho wa kuelekea katika klabu ya Ujerumani ya Hertha Berlin. (Blick, via Mirror)
Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta anataka kumsaini kiungo wa kati wa Adrien Rabiot, 24, kwa mkopo kutoka klabu ya ligi ya Seria A Juventus imwezi Januari. (Times - subscription required)
Mkufunzi wa Chelsea Frank Lampard anasema kwamba winga wa Brazil Willian 31 ameanza mazungumzo na klabu hiyo kuhusu kuongeza kandarasi yake ambayo inakamilika mwisho wa msimu huu.. (Mail)
Winga wa Manchester City Leroy Sane, 23, atasalia katika klabu hiyo hadi mwisho wa msimu huu lakini raia huyo wa Ujerumani anatarajiwa kuhamia Bayern Munich katika dau la £85m mwisho wa msimu huu . (Star)
Top 20 ya members wenye meseji nyingi kuliko wote jamii forums 1. RUTASHUBANYUMA(JF-Expert member) Message: 169,603 2. NUMBISA( JF-Expert member) Message: 151,963 3. MSHANA JR(platnum member) Message: 127,933 4. SHUNIE(JF-Expert member) Message: 118,537 5. SHIMBA YA BUYENZE( JF- Expert...