Kiungo wa Ajax na Uholanzi Donny van de Beek amehusishwa na kuhamia Manchester United lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22.(Fox Sports Netherlands, via ESPN)
Klabu ya Wolves inanafasi kubwa ya kumsaini Thomas Lemar wa Atletico Madrid kwa sababu ya uhusiano muzri wa Klabu hiyo na wakala wa mchezaji huyo wa Ufaransa mwenye miaka 22, Jorge Mendes.
(Mundo Deportivo, via Sport Witness)
Manchester United wako tayari kutoa wachezaji wawili, pamoja na beki wa Argentina mwenye umri wa miaka 29, Marcos Rojo, kama sehemu ya mpango wa pauni 60m kumsaini kiungo wa Ureno Bruno Fernandes, 25, kutoka Sporting Lisbon. (Talksport)
Manchester United wamethibitisha kumpa nafasi nyingine ya majaribio kiungo Boubakary Soumare, 20, kabla ya kumpa ofa kiungo huyo wa Ufaransa.(Sunday Express)
Sheffield United wanamfuatilia mlinzi wa kati wa Ipswich Town mwenye umri wa miaka 21, Luke Woolfenden, na klabu hiyo inampango wa kuwasaini mabeki wa kati wawili.(Sheffield Star)
Aston Villa na Newcastle United wako kwenye mapambano ya kumsaini mshambuliaji wa Le Havre Tino Kadewere, Norwich City na Tottenham pia wameonyesha kuvutiwa na mshambuliaji huyo wa Zimbabwe mwenye umri wa miaka 24. (Football Insider)
Mshambuliaji wa Kiingereza wa Crystal Palace, Connor Wickham, 26, anatarajiwa kujiunga na Sheffield Jumatano kwa mkopo kufuatia kuwasili kwa Cenk Tosun, 28, katika uwanja wa Selhurst Park. (Mail on Sunday)
Meneja wa Inter Milan Antonio Conte anasema alitaka kumsaini mshambuliaji wa AC Milan mwenye umri wa miaka 38 wa Sweden, Zlatan Ibrahimovic, ambaye alikuwa Manchester United wakati huo, nayeye akiwa bosi wa Chelsea. (Evening Standard)
Manchester United wanashindana na kiungo wao wa zamani David Beckham mmiliki Inter Miami kwa kumsaini kiungo wa Boca Juniors na timu ya tiafa ya Argentina mwenye chini ya umri wa miaka 20 Agustin Almendra,
He writes on his Twitter: " Xavi is now FC Barcelona's coach! All the details will be announced tomorrow (on Sunday), with his club Al Saad honouring and thanking him for his work at the club."
The date of his presentation and his first match as a coach for Barça will also be revealed.