Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwenye msimamo wa Ligi Kuu England msimu huu, Man United wapo nafasi ya tano huko, wameachwa nyuma kwa pointi 27 na vinara Liverpool, lakini kwenye ligi ya pesa, miamba hiyo ya Old Trafford, inazidiwa na timu mbili tu, tena sio za England
 
Huko kwenye Ligi Kuu England, Man City wanashika nafasi ya pili kwa kukusanya mkwanja mrefu, walipovuna Pauni 538.2 milioni, lakini wakishika nafasi ya sita kwa Ulaya, wakiwa mbele kwa nafasi moja dhidi ya mahasimu wao kwenye mbio za ubingwa, Liverpool, waliokusanya mapato ya Pauni 533 milioni.
 
Hata hivyo, wataalamu wa masuala ya kipesa wanaamini kwamba si muda mrefu, Man United itaenguliwa kwenye kilele hicho cha kuwa na mkwanja mrefu kutokana na mambo yao yanayoendelea uwanjani.
 
Kinachoelezwa, Man City ndio watakaowaondoa Man United kileleni kwenye ligi ya mkwanja. Deloitte inafichua kutakuwa na upungufu wa mapato kati ya Pauni 560 milioni hadi Pauni 580 milioni kwa msimu huu, kutokana na klabu hiyo kushindwa kuwamo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu wa pili.
 
Timu nyingine inayotishia kuwaondoa Man United kwenye kilele cha pesa ni Liverpool. Wababe hao wa Anfield wanacheza soka tamu kabisa kwa sasa na jambo hilo litawafanya kubeba mataji mengi yatakayowafanya kuvuna mkwanja mrefu.
 
Tottenham waliboresha kipato chao baada ya kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita, hivyo wanashika nafasi ya nane huko Ulaya wakiwa wameingiza kipato cha Pauni 459.3 milioni na Chelsea wapo kwenye nafasi ya tisa wakiwa wameweka kibindoni kipato cha Pauni 452.2 milioni.
 
Mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich walishika namba nne na Paris Saint-Germain walishika namba tano, huku Juventus wakikamilisha 10 bora na hakukuwa na nafasi yoyote kwa Arsenal katika hizo nafasi 10 za timu zenye mkwanja mrefu huko Ulaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…