STRAIKA, Marcus Rashford hakuwamo kwenye kikosi cha awali cha Manchester United kilichokusanyika kabla ya mchezo wao wa Ligi Kuu England dhidi ya Liverpool huko Anfield usiku Jumapili.
Fowadi huyo alikuwa na hatihati ya kukosa mechi hiyo kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya mgongo aliyopata kwenye mechi ya Kombe la FA dhidi ya Wolves katikati ya wiki iliyopita, hakuonekana wakati wachezaji wenzake walipokutana kukamilisha mambo ya mwishomwisho kabla ya kwenda Liverpool.
Wachezaji wa Man United walikutana kwenye hoteli ya Lowry iliyopo jijini Manchester, ambapo alitumia usiku wao wa Jumamosi hapo kujiandaa nna mchezo wao wa Anfield.
Wachezaji wote walikuwapo isipokuwa Rashford tu.
Taarifa hizo ni za neema kwa Liverpool, kutokana na ukweli kwamba Rashford amekuwa kwenye kiwango bora akifunga mabao 16 katika mechi 21 alizocheza tangu mara ya mwisho alipowafunga Liverpool katika mchezo uliofanyika Old Trafford, Oktoba mwaka jana.
Kumekuwa na ripoti kwamba Liverpool wameingia kwenye mchakamchaka huo wakitaka kuchuana na Chelsea katika mpango wa kunasa huduma ya Werner, ambayo inaripotiwa itapatikana kwa ada ya Pauni 60 milioni.
Werner ni moja ya washambuliaji moto kabisa huko Ulaya kwa sasa, akiwa anasakwa pia na vigogo Bayern Munich na Real Madrid ambao watachuana na klabu hizo mbili za Ligi Kuu England.
Kinachoelezwa ni kuwa Chelsea wamekuwa kwenye nafasi ya juu kabisa kumnasa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani, lakini Liverpool nao wanahitaji huduma yake.
Kocha Jurgen Klopp ni shabiki mkubwa wa fowadi huyo, ambaye amefunga mabao 20 katika mechi 18 za Bundesliga alizocheza msimu huu hivyo yupo tayari kwenda jino kwa jino na Frank Lampard ili kumpata mchezaji huyo, ambaye Jumamosi alifunga mara mbili kuipa timu yake ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Union Berlin.
MASHABIKI wa Manchester United wanasubiri kwa hamu kukamilika kwa dili la kiungo Bruno Fernandes, lakini unaambiwa hivi bonasi ndiyo inayochelewesha dili hilo kukamilika hadi sasa.
Kiungo huyo fundi wa mpira, Fernandes, 25, alicheza mchezo wa juzi Ijumaa wakati chama lake la Sporting Lisbon lilipomenyana na Benfica na mashabiki wake wanaamini huo pengine ndiyo ulikuwa mchezo wa mwisho kwake kuvaa jezi za timu yao.