Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Bale-Benzema -Hazard

Utatu huu umecheza pamoja mara nne tu, kwa mara ya kwanza watatu hawa kuongoza mashambulizi ya Real Madrid ilikuwa katika mechi dhidi ya Granada ambapo Madrid ilishinda kwa mabao 4-2, kisha timu hiyo ikafungwa na Paris Saint Germain kwa mabao 3-0.
 
Vazquez-Benzema-Hazard

Utatu huu umeiongoza Real Madrid katika mechi mbili tu dhidi ya moja dhidi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Club Brudge nyumbani iliyomalizika kwa sare ya 2-2 na nyingine ni ya ugenini La Liga dhidi ya Eibar timu hiyo ikashinda kwa mabao 4-0.
 
Rodrygo- Benzema -Vinicius

Benzema alimewahi kuzungukwa na watoto hawa wa Kibrazili mara mbili tu, hii ilikuwa katika dhidi ya Espanyol ilioshinda kwa mabao 2-0 na katika mechi ambayo ilitoka suluhu na Atletic Bilbao, utatu huu ni moto lakini unahitaji muda zaidi kuaminika.
 
Bale- Benzema-Vinicius

Katika harakati zake za kuendelea kujaribu ni utatu gani unaweza kuirudisha Real Madrid katika utawala wake Zidane amewahi kujaribu kuwatumia Bale-Benzema na Vinicius kwenye mechi dhidi ya Celta Vigo ugenini na timu hiyo ilishinda kwa mabao 3-1.
 
Jovic- Benzema-Bale

Luka Jovic ameshindwa kuonyesha kiwango chake halisi tangu asajiliwe na Real Madrid wakati wa kiangazi mwaka jana, Zidane aliwahi kujaribu kumtumia pamoja na wakongwe Bale na Benzema hii ilikuwa katika mechi ya sare ya 2-2 dhidi ya Villarreal na tangu siku huyo kocha huyo hajawahi kuwatumia pamoja tena.
 
Vazquez-Benzema -Vinicius

Majaribio ya Zidane yamewahi kuwaweka kwenye kikosi cha kwanza pamoja Lucas Vazquez, Benzema na Vinicius utatu unaokupa kasi (Vazquez), utulivu na jicho la goli (Benzema) na ufundi, burudani na chenga za maudhi (Vinicius), watatu hawa wamewahi kucheza pamoja katika mechi dhidi ya Levante tu siku ambayo Real Madrid ilishinda kwa mabao 3-2 nyumbani.
 
Vazquez-Jovic- Vinicius

Huu ni utatu mwingine ambao Zidane ameujaribu msimu huu, Vazquez, Jovic na Vinicius walicheza pamoja katika pambano ambalo Real Madrid iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Osasuna katika Uwanja wa Santiago Bernabeu.
 
Rodrygo- Jovic-Vinicius

Utatu huu ulitumika katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Club Brugge ugenini na madogo hawa hawakumuangusha Zidane kwa sababu waliiongoza timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 huku Rodrygo akifunga bao moja na kumtengenezea Vinicius jingine huku bao la tatu kwenye mechi hiyo likifungwa na mkongwe Luka Modric.
 
Vazquez-Jovic- Rodrygo

Hawa walicheza pamoja katika mechi dhidi ya Sevilla nyumbani na kuipa Madrid ushindi wa mabao 2-1, licha ya kuwa hawakufunga bao kwenye mechi hiyo, lakini Jovic alitoa pasi ya bao la kwanza kwa Casemiro na Vazquez akampa Casemiro pasi ya bao la pili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…